Akizungumza wakati akikabidhi saruji hizo kwa viongozi wa serikali za vijiji na mitaa Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika amesema kusitokee mtu akarudia kuuza ama kuhifadhi vibaya hadi zikaharibika na badala yake ziendee moja kwa moja kukamilisha maboma yaliyoanzishwa na wananchi.
Amesema Mahitaji ya saruji kwa ajili ya kukamilisha maboma na vifaa vingine vya ujenzi ni makubwa sana lakini mifuko 1200 kutoka kwenye mfuko wa jimbo na nyingine kutoka kwenye mshahara wake utasaidia kupunguza mahitaji .
Kwa upande wao viongozi waliyowakilisha wananchi kupokea mifuko hiyo ya saruji Innocent Mlange mkiti Nundu wamesema katika vijiji na mitaa yao kuna miradi mingine imeanzishwa na wananchi na kisha kuishia njiani hivyo saruji hizo zinakwenda kuwapunguzia mzigo wananchi kuchangia na kisha kuahidi kutumia kama mfuko wa jimbo unavyohitaji.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpte na Philoteus Mligo diwani wa Lugenge wametoa maelekezo kwa vijiji na mitaa yote iliyopatiwa saruji hizo ,wakitaji kulinda ili isiharibike na kwamba kuna miradi inahitaji saruji hizo na vifaa vingine taarifa zitolewe mapema kwani kuacha mifuko hiyo kwa muda mrefu inaweza kuharibika.