RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliofanyika leo 20-4-2024 katika ukumbi wa Hoteli hiyo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Masoko wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC)Ndg.Nurdin Hussein Mohamed,wakati akitembelea maonesho katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya PADDCO Ndg. Afla Abdalla Mrusi,wakati akitembelea maonesho ya Wahandisi katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, kabla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Mohamed Salum na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Al Hatmy Desigh&Engineering Consultancy Zanzibar Ndg.Abdulhamid Mohammed Ali Mhoma akitowa maelezo ya michoro ya majengo inayojenga kampuni hiyo Zanzibar,wakati akitembelea maonesho ya Wahandisi katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, kabla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Mohamed Salum na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza akimsikiliza Mwanafunzi wa Chuo cha Karume Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume Zanzibar, akitowa maelezo ya ufundi wa utengenezaji wa mashine za ndege,wakati akitembelea maonesho ya Wahandisi katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, kabla ya Kuzindua Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Mohamed Salum na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt.Mngereza Mzee Miraji.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza akimsikiliza Mwakilishi wa Rak Mhandisi Mbarouk Masoud Mbarouk , akitowa maelezo ya vifaa vya ujenzi,kabla ya Kuzindua Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji,uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Mohamed Salum na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt.Mngereza Mzee Miraji na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wahandisi,Wasanifu na Wakadiriaji wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuizindua Taasisi hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 20-4-2024.(Picha na Ikulu)
………………..
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inathamini sana mchango wa
fani za Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Zanzibar kwenye utekelezaji wa
mipango mikubwa ya Maendeleo hasa miradi ya ujenzi.
Imesema itaendelea kuwahusisha kikamilifu kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa
ya maendeleo kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji wa wataalamu wa Kitanzania
katika miradi endelevu ya kimkakati ya uwekezaji nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
ameyasema hayo alipozindua taasisi ya wasanifu, wahandisi na wakadiriaji
Zanzibar, kwenye ukumbi wa hoteli Verde, Mtoni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini
Magharibi.
Amesema, kwa kiasi kikubwa Serikali ilijitahidi kuzitumia kampuni za ndani kwenye
ujenzi wa miradi mbalimbali hasa wakati wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya fedha
za UVICO zilitumika kampuni za ndani (wazawa) kwa lengo la kuwajengea uwezo ili
wapate miradi mikubwa zaidi. Pia, Rais Dk. Mwinyi alieleza miradi yote ilikamilika
kwa ufanisi hali ya juu zaidi.
Alisema, Serikali zote mbili za (SMZ) na (SMT) zinafanya jitihada za makusudi
kushirikisha taaluma hizo kwenye shughuli tofauti za maendeleo, ikiwemo
kuweka mazingira yanayowawezesha kujiajiri, kuhamasisha utambuzi wa fursa
mbalimbali kupitia rasilimali zilizopo nchini pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya
kufanikisha utafiti na ubunifu mbalimbali.
“Tunajua tunahitaji kushirikiana ili kufanikisha dhamira ya Maendeleo Endelevu
hususan fani hizi kutokana na umuhimu wake kwa ustawi wa nchi yetu”. Alieleza
Rais Dk. Mwinyi.
vilevile Dk. Mwinyi alieleza hizo ni uti wa mgongo wa shughuli nyingi za uchumi wa
nchi kwani zinabeba dhima ya shughuli-mama katika harakati za kujenga,
kuimarisha na kuendeleza maendeleo ndio maana Serikali inazipa mazingatio
makubwa.
Alisema Serikali pia imefungua njia kwa fani hizo kuwa na uthubutu na kujiamini
sambamba na kuwasihi wahandisi hao kuendelea kuongeza juhudi ili kazi zao zizidi
kuchangia kiasi kikubwa cha kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Dk. Mwinyi alisema Tanzania ni nchi inayoendelea na inajivunia kufikia Uchumi wa
Kati, kutokana na kuwa na miradi inayochangia zaidi pato la Taifa, nyuma yake
wakiwepo wenye fani za usanifu, uhandisi na ukadiriaji wa ujenzi.
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi alieleza, Serikali ya Zanzibar kupitia Uchumi wa Buluu
imeendeleza Sera ya kuajiri wasanifu, wahandisi na wakadiriaji wazalendo ikiamini
kuna wakandarasi wazuri na washauri elekezi mahiri (wazawa) wenye uwezo
mkubwa wa kufanyakazi za uhandisi kwa weledi kupitia miradi mbalimbali
waliyoitekeleza kwa ufanisi mkubwa ni kielelezo cha kuaminika kwao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Dk.
Khalid Salim Mohamed amesema Sekta ya majengo na ujenzi Zanzibar iko kwenye
mageuzi makubwa kwa kasi kubwa ya ujenzi inayoendelea nchi nzima zikiwemo
barabara za mijini na vijijini, ujenzi wa skuli za ghorofa maeneo yote ya visiwa vyaUnguja na Pemba, ujenzi wa hospitali kwa wilaya zote nchini ujenzi wa nyumba za
makaazi miundombinu ya maji safi na salama pamoja na umeme.
Alisema hatua hiyo inatokana na dhamira njema na maono ya Rais Dk. Mwinyi
katika azma yake ya kuibadilisha Zanzibar na mandhari na haiba nzuri ya
maendeleo endelevu.
Alizipongeza juhudi za wahandisi wote kwa ushiriki wa wao mkubwa wa mageuzi
yanayoendelea nchini chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi, kupitia sekta ya ujenzi na
miundombinu.
Alisema, maisha ya kila siku yanategemea mchango na ushiriki mkubwa wa
wahandisi.
Dk. Khalid alifafanua makaazi ya watu wanayoishi, ofisi na mawasiliano yao, nishati
za umeme, madaraja na barabara wanazozitumia, maji safi na salama na shughuli
zote za jamii zina mnasaba mkubwa na kazi za wahandisi.
Hivyo, alileleza kuundwa kwa taasii ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Zanzibar
ni kielelezo muhimu cha kukuza uwezo wao katika kuimarisha sekta ya ujenzi kwa
maendelo ya nchi.
Naye, Rais wa Taasisi ya Wasanifu Wahandisi na Wakadiriaji Zanzibar, QS.
Abduswamad Mohamed Mattar amesema taasisi hiyo ilimedhamiri kufanya
makubwa zaidi kama mchango wao kwa taifa na kuadhimia kuwa na wanachama
wengi ambapo kwa sasa kuna wanachama 192. Hivyo. Aliwashauri wataamu wa fani
hizo kuendelea kushirikaina na kujiunga kwa wingi wao ili kushajihishana zaidi.
Aidha, alieleza kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na taaasiisi mbalimbali za
ujenzi ndani na nje ya nchi ikiwemo kutayarisha mafunzo nao kujifunza zaidi mageni
wasiyoyajua sambamba na kusaini hati tofauti za makubaliano kwa taasisi
mbalimbali za wahandizi bara na visiwani.