Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel nchimbi, amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanachama na viongozi kuwa na nongwa jambo ambalo linapelekea kupoteza upendo, umoja na mshikamano na kutengeneza makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameyasema hayo kwenye mkutano wa ndani uliokutanisha viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia ngazi ya mashina, Viongozi wa Serikali, Taaisi zisizo za kiserikali, Wazee na Viongozi wa dini.
“Umoja kwa wanachama na viongozi na jambo la muhimu na kwa kadri inavyowezekana muhakikishe suala hilo linakuwa la msinhi na kwanza baina yenu”
“Tukienda kwenyebchaguzi zetu na tukimaliza chaguzi mambi ya huko yaishe, msijikite katika kuendelea nayo”
“Nongwa za uchaguzi ziishe , unakuta chaguzi zimeisha miaka 4 iliyopita lakini unakuta mtu bado ana nongwa kuanzia aliyeshinda hadi aliyeshindwa, hatuwezi kujenga chama cha watu wenye nongwa”
Aidha, Amepongeza tabia ya baadhi ya viongozi na wanachama kuwa na msimamo na kutoyumbishwa daima na badala yake kusimamia kwenye kuzingatia katiba na miongozo ya chama cha mapinduzi”