Uwepo wa Mabweni katika shule za sekondari zimeelezwa kuwa ni moja ya kichocheo cha wanafunzi wa kike kufanya vizuri kwenye masomo yao na kuepukana na vishawishi ambavyo vimekuwa vikiwapelekea kushindwa kutimiza ndoto zao.
Akizungumza kwenye mahafari ya pili ya kidato cha sita kwenye shule ya Sekondari ya Shantamine iliyopo kata ya Mtakuja,Halmashauri ya Mji wa Geita,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa Kata hiyo,Constantine Molandi,amesema suala la uwepo wa mabweni umesaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao kutokana na kupata muda mrefu wa kujisomea.
“Ukweli uwepo wa mabweni umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kuboresha suala la elimu hususani kwa watoto wa kike ukiangalia zamani watoto wengi walishindwa kufikia ndoto zao za kimasomo kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata elimu lakini leo hii mfano mzuri ni hapa shantamine watoto wamekuwa wakifurahia na kufanya vizuri kwenye masomo yao kutokana na uwepo wa mabweni na sisi kama halmashauri ni kuona tunaongeza Mabweni mengi zaidi ambayo yatachochea elimu kwa watoto wetu”Constantine Molandi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Nao wazazi na walimu wameelezea umuhumu wa uwepo wa mabweni shule ambavyo umeendelea kuwa chachu ya ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
“Ufaulu shuleni hapa umekuwa ukiongezeka kila mwaka kwanza uwepo wa kidato cha tano na sita kwetu imekuwa ni fursa kwa wanafunzi wa madarasa ya kuanzia kidato cha kwanza hadi na cha nne wamekuwa wakitumia kama fursa ya wao kufundishwa masomo ambayo wanaona wanaweza kufundishwa na wanafunzi wenzao”Kakila Swila .Mwl Mkuu wa shule ya Sekondari ya Shantamine.
“Sisi wazazi kwetu imekuwa ni faraja kubwa kuona watoto wetu wanafanya vizuri kutokana na uwepo wa mabweni ya shule ya Sekondari Shantamine”Yohana Mathias,mzazi .
Nao wanafunzi wa kidato cha Sita wa shule hiyo ambao wanatarajia kuanza mtihani wao wa kuhitimu kidato cha sita tar 6 mwezi wa tano wameelezea namna walivyojianda kukabiliana na mtihani huo.
“Tunashukuru sana kwa maandalizi mema ambayo walimu wetu wametupatia tunauhakika wa kufanya vizuri pindi tutakapokwenda kufanya mtihani wetu wa kuhitimu kidato cha sita tunamatumaini makubwa ya kwenda kufanya vizuri”Elina Dison,Mwanafunzi kidato cha Sita Shantamine.