Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakishiriki semina ya kujengewa uwezo iliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyofanyika Aprili 17, 2024 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu uliopo kurasini, Wilaya ya Temeke, Dar es Saalam.
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Temeke, David Mhando akizungumza na watumishi wa mkoa huo wakati akifungua semina ya kujengewa uwezo iliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyofanyika Aprili 17, 2024 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu uliopo kurasini, Wilaya ya Temeke, Dar es Saalam.
Afisa Mwandamizi wa Rasilimali Watu na Utawala TANESCO Mkoa wa Temeke, Jumanne Songoro akizungumza na watumishi wa mkoa huo katika semina ya kujengewa uwezo iliyotolewa na , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyofanyika Aprili 17, 2024 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu uliopo kurasini, Wilaya ya Temeke, Dar es Saalam
Afisa wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,Bw. Hamadi Bakari akitoa mada katika semina ya Watumishi wa mkoa huo iliyofanyika Aprili 17, 2024 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu uliopo kurasini, Wilaya ya Temeke, Dar es Saalam.
Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakisaini hati ya uadilifu kwa watumishi wa umma.
……
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wamejengewa uwezo na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia uadilifiu, uwajibikaji, uwazi pamoja na kufata masharti ya sheria ya maadili katika utekelezaji wa majukumu.
Akizungumza Aprili 17, 2024 kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, wakati akifungua semina kwa watumishi wa TANESCO Mkoa wa Temeke iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu, Kurasini jijini Dar es Salaam, Mhandisi Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Temeke, David Mhando, amesema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa watumishi wa TANESCO katika kuaendelea kutekeleza majukumu kwa uweledi.
Mhandisi Mhando amesema kuwa jukumu la TANESCO ni kuzalisha umeme, kusafirisha pamoja na kusambaza, hivyo kama watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na usawa ili kuleta tija kwa shirika na Taifa.
“Shirika la TANESCO lina utaratibu kutoa semina kwa watumishi wake kwa lengo la kuwaelimisha ili waweze kufanya kazi yenye kuleta tija na maendeleo kwa Taifa“ amesema Mhandisi Mhando.
Akitoa mada kwa Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Afisa wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Hamadi Bakari, amesisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kufanye kazi kwa bidii, weledi, nidhamu, uadilifu na ubunifu ili kutimiza maono ya Serikali ya kuwaletea maendeleo watanzania.
Bw. Bakari amesema kuwa kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu, mipango na mikakati wanayoisimamia yanahitaji juhudi ya kila mtu kwa kuzingatia nidhamu katika kufanya kazi.
“Kila mtumishi anapaswa kuzingatia nidhamu ya kazi na maadili ya utumishi wa umma, watumishi wa umma mnao wajibu wa kufuata na kutekeleza misingi ya kazi kwa ufasaha ” amesema Bw. Bakari.
Amesema kuwa kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi ikiwemo stahiki mbalimbali, ulipaji wa malimbikizo ya mishahara, kuongeza posho ni muhimu katika kuongeza hamasa ya kufanya kazi kwa uweledi.
Amewakumbuwa watumishi wa tanesco mkoa wa temeke kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ili waweze kufanikiwa kutekeleza ipasavyo majukumu ya shirika kwa ufanisi wa hali ya juu.
“Tuwe wazalendo wa nchi, utii kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kulinda mazingira na mali za umma pamoja na kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote” amesema Bakari.
Katika semina hiyo Afisa wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Hamadi Bakari amesimamia zoezi la watumishi wa tanesco mkoa wa temeke kusaini hati ya uadilifu kwa watumishi wa umma.