Na Abel Paul,Jeshi la Polisi Moshi Kilimanjaro.
Shirikisho la Wakuu wa Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afriks wameungana na Polisi wenzao kutoka Nchini Rwanda kuuwakumbuka Wananchi waliopoteza maisha katika mauaji ya kimbari Nchini Rwanda mwaka 1994.
Akiongea leo Aprili 14,2024 katika Shule ya Polisi Tanzania Mkoani Kilimanjaro Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Wakuu Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afrika na Mkuu wa Interpol Kanda ya Afrika Mashariki Apollo Afrika amesema wamekuwa wakifanya maadhimisho ya kumbukumbu ya wananchi waliopoteza maisha katika mauaji ya kimbari yaliyotokea miaka 30 iliyopita nchini Rwanda.
Mkurungenzi Huyo mbali na kubainisha hilo amesema wanatumia kumbukumbu hiyo kama funzo kwa wananchi wengine kutojiingiza katika ubaguzi wa ukabila ambapo alibainisha kuwa kipindi cha maauji hayo nchini Rwanda yalikuwa ni yakitisha na yalichafua taswira ya Nchi hiyo.
Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime pamoja na kushiriki kumbukumbu hiyo amewataka waandishi wa habari kuzingatia Maadili katika kuwahabarisha wanaanchi ili kuepusha taharuki na migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama katika maeneo ya ukanda huo.
Nao baadhi askari walioshiriki kumbukumbu hiyo iliyofanyika shule ya Polisi Tanzania TPS Moshi Kilimanjaro wamebainisha kuwa wametumia siku hiyo kuwa kumbuka na kuwaombea wananchi waliofariki katika mauaji ya kimbari Nchini Rwanda.