Raisa Said,Bumbuli
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Bumbuli January Makamba Amesema kwenye Chama Cha Mapinduzi CCM kumekuwa na mambo ya kufitiniana hasa pale Rais aliyepo madarakani anapotakiwa kuendelea na muhula wa pili.
Hayo ameyasema kijijini kwao Mahezangulu Halmashauri ya Bumbuli Mkoani Tanga wakati wa Maulidi ya 40 inayofanyika kila Mwaka siku ya idd pili kijijini hapo ya kuwaombea ndugu zao waliotangulia mbele za haki.
Makamba alisema chanzo kikubwa Cha kufitiniana ni wanapokuwa na Rais anae stahili kuendelea kuongoza Kipindi Cha pili nakwamba katika nyakati hizo watu ndani ya chama hicho hufitiana hasa.
” Kama vile ada kwenye ccm watu wakitaka kufitiniana wanasema unamuona yule bwana hataki huyu aendelee,unamuona yule bwana ana njamanjama ili huyu aonekane hafai,unamuona yule bwana anatega huyu ashindwe ndo tulivyo “Alisisitiza Makamba nakuongeza kuwa wakati siku zote huamua” alieleza Makamba
” Ndugu zangu tuendelee kuombeana fitina hizi zisiwe na mashiko kwenye nchi yetu na kwenye Chama chetu ,nazitakoma siku ile sa kumi jioni mgombea wa kiti Cha Urais kupitia CCM atakapokuwa kachukua mtu mmoja pekee kutoka ndani ya CCM ambaye ni Rais Samia” Alisema Makamba.
Waziri Makamba amesisitiza kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani mgombea pekee atayegombea nafasi hiyo ya kiti Cha Urais ni Rais Samia kama ilivyo utaratibu wa siku zote Wa chama hicho.
Waziri Makamba alisisitiza kuwa nchi ya Tanzania imebarikiwa kupata Rais anaye ongoza vizuri kwa busara na hekima nakwamba hiyo imepelekea nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu .
Hata hivyo alitumia jukwaa hilo kueleza hatua ya kuongozwa na Rais Samia kuwa ni baraka kwa kuwa ni kiongozi mwenye busara na hekima mambo yanayochagiza Maendeleo ,amani na utulivu wa nchi.