Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
Walimu wakuu na wakuu wa shule za sekondari wilaya ya Nachingwea wametakiwa kuingia mikataba na wazazi hadi tarehe 30/04/2024 ili kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi watoro.
Akizungumza wakati wa kikao cha tathimini ya elimu kwa robo ya mwaka kuanzia Januari hadi Mwezi wa tatu kwa walimu wakuu na wakuu wa shule na waratibu elimu kata wa wilaya ya Nachingwea, Afisa elimu mkoa wa Lindi Mwalimu Joseph Mdeo amewataka viongozi hao kusimamia ipaswavyo zoezi la kuingia mikataba na wazazi kwa ajili ya kusimamia nidhamu na kuzuia utoro kwa mwanafunzi na atakaefanya utoro basi mzazi atawajibika
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila alisema kuwa atazungumza na Madiwani waweze kutembelea shule kufuatilia maagizo waliyopewa kama yanatekelezwa
Mpyagila aliwashauri kwenye shule wawepo na wazibiti ubora na wawe na mafaili yao kwani wamepewa maagizo na afisa elimu wa mkoa kutembelea katika shule zote.
Naye Mkurungezi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa amewataka mafisa elimu kusikiliza maoni ya waalimu wakuu kwenye msawazo wa walimu ujao ili kupeleka waalimu kutokana uhitaji wa shule husika.
Aidha mkurugenzi Kawawa alisema kuwa kwenye maeneo yenye changamoto ya wanyama tembo Halmashauri inafanya jitihada mbalimbali na wameiandikia serikali kuu kuomba ujenzi wa hosteli katika maeneo hayo. Amesem wamepata wadau ambao ni UNICEF na WWF na tayari wameonesha nia ya kujenga hosteli.