MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kuwasili mkoani Tanga Aprili 9 mwaka huu ukitokea mkoani Kilimanjaro ambapo utazinduaa miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 40 na utakimbizwa kwenye Halmashauri 11 za mkoa wa Tangaa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Mwenge huo utapokelwa mkoani humo ukitokea Mkoani Kilimanjaro ambapo mapokea yatafanyika kwenye Kijiji cha Mazinde wilaya ya Korogwe ambapo utakagua na kuweka mawe ya msingi miradi 87.
Ambapo aalisema kqwamba mwenge huo unatarajiwa kukimbizwa umbali wa kilomita 1635 na na baada ya kupitia miradi na kuikaagua na baada ya kumaliza mbio zake mkoani hapa utakabidhiwa mkoani Morogoro
Aidha alisema kwamba fedha hizo zipo kwenye mchanganuo wa Bilioni 40.9,Nguvu za wananchi ni Milioni 196.8 ,Halmsahri Bilioni 1.8,Serikali Kuu Bilioni 20.8, Fedha za wahisani bilioni 18.4 ambazo zimepelekea kuwepo kwa idadi hiyo wa fedha hizo.
“Ujumbe maalumu wa Mwenge mwaka huu ni tunza mazingira mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu kwa hiyo tunategemea kwenye miradi ya mwenge kutakuwa na utunzaji wa mazingira ,kutakuwa na kutakuwa na ujumbe wa kupiga vita Dawa za Kulevya”Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba Pamoja ana ujumbe huo mwenge wa uhuru utaendelea kuhamasisha na kuwaelimisha wananchi juu ya mapambano dhidi ya Rushwa,Malaria,VVU /UKIMWI,Dawa za Kulevya na uzingatiaji wa Lishe bora.
Hata hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuulaki mwenge wa uhudu katika mapokezi,barabarani,kwenye miradi na maeneo ya mikesha