Kamanda Senga amesema “Jeshi la Polisi limeendelea na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia vinatokomezwa katika jamii hivyo wazazi/walezi mnatakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa ya vitendo hivyo pindi muonapo au mfanyiwapo ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya doria za kiroho ili jamii ibadilike na ichukie vitendo hivyo kwa lengo la mkoa wetu kuwa salama” alisema Kamanda Senga.
Aidha, Kamanda Senga aliongeza kuwa “Mnapaswa kuwasimamia watoto wadogo kwani kwa umri walionao hawawezi kujisimamia na kufanya maamuzi, wanahitaji njia na miongozo ili waweze kufikia malengo ya masomo yao sasa basi mzazi/mlezi ni jukumu lako na jamii kwa ujumla kuwaongoza watoto kwa yale yaliyo mema kama kumfundisha na kuja naye kanisani ili amjue Mungu mapema kwa kufanya hivyo tutatengeneza kizazi kilicho bora na kisicho na mmomonyoko wa maadili katika taifa letu”
Sambamba na hilo, Kamanda Senga amewataka waumini wa Kanisa hilo kutumia maneno kutoka kwenye Biblia Takatifu kuwakumbusha waumini hao kuacha kutoa rushwa kwa watumishi wa serikali kupitia Kutoka 23:8 “Nawe usipokee rushwa, kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki”.