Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amewataka RUWASA kuzingatia usalama wa makazi ya wananchi wanaozunguka mradi wa maji skimu ya Lawate Fuka (Gararagua – KIDECO) lenye tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 100,000.
Ameyasema leo Aprili 4,2024 wilayani Siha kwenye uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa skimu ya maji ya Lawate – Fuka wenye gharama ya Tshs. Bilioni 2.3
Mnzava amesema mradi huo umezungukwa na makazi ya watu hivyo ni jukumu la RUWASA kuweka uangalizi wa karibu katika matanki hayo yasijekuleta madhara katika makazi ya watu hata hivyo, amepongea RUWASA kwa mradi mzuri utakaohudumia wakazi wapatao 7,828 wa vijiji vya Sanya juu, Merali na Ngumbaru.
Akisoma taatifa ya mradi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mhandisi Emmy George Meneja wa RUWASA wilaya ya Siha amesema mradi huo umehusisha shughuli za ununuzi wa bomba lenye urefu wa Mita 28,800, uchimbaji wa mtaro, kulaza Bomba na kufunika mtaro wenye urefu wa mita 28,800, ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 100,000, ujenzi wa vituo 4 vya kuchotea maji, ujenzi wa matanki 5 ya kupunguza nguvu ya maji (BPT), na ujenzi wa chemba 93.