Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Godfrey Mnzava amezindua jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali maalumu ya Taifa ya magonjwa ambukizi Kibong’oto Aprili 4, 2024 na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Timbuka kwa kusimamia vyema ukarabati wa jengo hilo linye uwezo wa kuhudumia wagonjwa mahututi 20 kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, hadi kukamilika kwa ukarabati wa jengo hilo limegharimu kiasi cha Tshs. Bilioni 1.3 ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa tiba na mafunzo kwa wataalamu
Vile vile kazi mbalimbali zimefanyika Katika ukarabati wa wa jengo hilo kazi zilozofanyika ni kama kuezua paa, kuvunja kuta za tofali pamoja na sakafu, kujenga baraza ya mbele, kumwaga jamvi, kujenga kuta, kuweka sakafu ya tarazo, kupaua,kuweka mifumo ya umeme na hewa ya oxygen, kuweka mfumo wa TEHAMA pamoja na kununua vifaa tiba mbalimbali.