Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe Mudrik Ramadhani Soraga akitoa wasifu wa Marehemu Kanal Mstaafu Said Iddi Bavuai katika kaburi lake huko Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja wakati wa kufanya ziara na kusoma dua.ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa .na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Muongozaji dua Sheikh Sharif Abdulrahman wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar akisoma dua ya Marehemu Kanal Mstaafu Said Iddi Bavuai katika kaburi lake Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja wakati wa kufanya ziara na kusoma dua,ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar .
Mmoja wa Mwanafamilia Rukia Saidi Iddi Bavuai akitoa shukrani Kwa niaba ya familia ya Said Bavuai huko Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’katika Kaburi la Marehemu Kanal Mstaafu Said Iddi Bavuai wakati wa kufanya ziara na kusoma dua .ikiwa niI Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.
………………………..
Na Khadija Khamis ,_Maelezo .01-04-2024
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Mudrik Ramadhani Soraga amesema Kanali Mstaafu Marehemu Saidi Iddi Bavuai alikuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa Nchi sio kwa kuhadithiwa bali alikuwa mpambanaji katika kuupigania Uhuru wa Zanzibar .
Akitoa kauli hiyo huko Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja wakati wa kufanya ziara na kusoma dua katika kaburi la kanal Mstaafu Marehemu Saidi Iddi Bavuai .
Amesema Marehemu alikuwa nI kiongozi wa kupigiwa mfano Kwa namna ambavyo ameitumikia Nchi na Serikali yale.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Kwa kuthamini juhudi za viongozi mbali mbali waliokwisha tangulia mbele ya haki imeamua kuandaa ratiba maalumu ya kila mwaka kuyatembelea makaburi yao na kuwaombea dua pamoja na kupata fursa ya kukutana na wanafamilia.
Alifahamisha kuwa viongozi waliotangulia walithaminiwa na Serikali za Awamu zote zilizopita na kuamini kwamba wataendelea kuthaminiwa na kuombewa dua Kwa kila mwaka .
Nae Mmoja wa Wanafamilia Rukia Saidi Iddi Bavuai akitoa shukrani Kwa niaba ya familia amesema ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kwa kuandaa utaratibu huo wa kuonana na viongozi katika dua ya pamoja ya Mzee wao
Amesema kushirikiana pamoja katika dua ya Mzee wao kunasaidia kujenga Imani na umoja katika familia na Serikali Jambo ambalo litaimarisha udugu na mshikamano.
Kwa Upande wa Muongozaji wa dua Sheikh Sharif Abdulrahman wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar akiongoza dua ya Marehemu Kanal Mstaafu Saidi Iddi Bavuai na kumuomba Mwenyezi Mungu amughufirie madhambi yale na ampe Pepo ya daraja la juu , Amin .
Ziara na dua za viongozi ni Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa chama cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Aman Karume