Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba
………………………
Raisa Said,Bumbuli
Hatimaye kilio cha muda Mrefu Cha Wakazi wa Bumbuli kuhusu barabara yao ya soni- Bumbuli hadi Dindila wilayani Korogwe yenye urefu wa kilometa 74 kuanza kupatiwa dawa mwezi huu
Ni baada ya Waziri wa Ujenzi Innosent Bashungwa kusema Rais wa Jamhuri Wa Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametoa kibari cha kuanza kutangaza tenda ya kumpata Mkandarasi atakayejenga kilometa 30 kwa kiwango cha lami katika barabara hiyo.
” Tunatarajia kutangaza mwezi huu Wa nne maana Rais Samia ameshatoa kibari cha kutangaza tenda ya kumpata Mkandarasi atayejenga kilometa 30 kwanza za barabara hiyo” Alisema Bashungwa mara baada ya kupigiwa simu na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba wakati wa Mkutano wake na wananchi wa Jimbo hilo.
Waziri Bashungwa aliwahakikishia wakazi wa Bumbuli kuwa tangazo Hilo litatoka Mwezi huu wa nne nakwamba yale mambo tuko kwenye mchakato tupo kwenye upembuzi yakinifu yamekwisha sasa tunaanza mchakato wa kumpata mkandarasi atayejenga barabara hiyo
Akizungumza mara baada ya simu hiyo ya Waziri wa Ujenzi ,Makamba alieleza kuwa anamshukuru Rais Samia kwa uamuzi wake Wa kuamua tenda itangazwe kwaajili ya kumpata Mkandarasi lakini kwa kuamua kutenga rasilimali kwaajili ya jambo hilo.
Makamba alisema kilio kikubwa Cha Wanabumbuli ni barabara nakwamba barabara hiyo itakapo jengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami itapitika wakati wote na itazidi kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Halmashauri kwa ujumla.
Waziri Makamba yuko jimboni kwake kwa ziara ya siku moja ambapo amekutana na kufanya mkutano na wananchi wake wa Bumbuli.