Shekhe Iddi Ngela ambaye ni Kiongozi wa dini Arusha akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha.
Shekhe Haruna Hussein akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika kikao hicho na viongozi wa dini
…………
Happy Lazaro, Arusha
Baadhi ya viongozi wa dini mkoani Arusha wamempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka mitatu madarakani na kufanikiwa kutekeleza miradi mkubwa ya kimkakati yenye maslahi mapana na Taifa.
Wakizungumza jijini Arusha waandishi wa habari viongozi hao pamoja na mambo mengine wamezungumzia miradi mikubwa ambayo imefanywa na Rais Samia kwenye sekta ya utalii hususani baada ya kuzinduliwa kwa filamu ya kutangaza utalii ya The Royal Tour.
Shekhe Iddi Ngela ambaye ni Kiongozi wa dini Arusha amesema kuwa, Rais Samia amefanya mambo makubwa sana katika kipindi cha miaka mitatu ambayo ni mfano wa kuigwa kwa viongozi waliopo madarakani katika kuhakikisha wanamuunga mkono na kuyaendeleza yale yote anayoyafanya.
“Kila mmoja anaona namna ambavyo Rais Samia amefanya mambo mengi na makubwa kwa kipindi cha miezi mitatu na ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunayaendeleza hayo yote ili kuendelea kuchochea kasi ya maendeleo. “amesema.
Kwa upande wake Shehe Haruna Hussein amesema kuwa ,tangu Rais Samia apewe nchi amefanya mambo makubwa sana na ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunakuwa na safari ya kumpongeza kwa yale yote aliyoyafanya kwani ameonyesha ujasiri mkubwa katika kuiongoza nchi.
Aidha amewaomba wanasiasa waendelee kumuunga mkono Rais katika utendaji kazi wake ili aendelee kuwahudumia watanzania kwa amani na utulivu mkubwa.
Aidha amewataka viongozi mbalimbali wa siasa kuhakikisha wanapendana na kuwa wamoja huku akionya tabia yao kuacha kungangania madaraka na nafasi mbalimbali na kamwe wasitamani kukaa kwenye kiti muda mrefu hadi kiwazoee.
“Hatutakiwi kumlaumu Rais kwa chochote bali kwa pamoja tunapaswa kuungana na kumpongeza kwa pamoja kwani mambo aliyoyafanya ni makubwa sana na kila mmoja anajionea , hivyo tuendelee kumuunga mkono kwa kila jambo.”amesema.
Naye Shehe Abubakari Kundia amewataka viongozi wa dini kuungana kwa pamoja katika kuzungumzia utalii wenye hadhi ili kuendelea kuvitangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi na hatimaye kuweza kupata watalii zaidi .