Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imemhukumu Bw. NASWIRU MPENDEKELAKI, Mwalimu wa Shule ya Msingi Kahaazi na mmiliki wa Mpendekelaki stationary.
Mshitakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi 500,000/= au kwenda jela miaka 2 kwa kuomba na kupokea hongo ya shilingi 300,000/= kinyume na k/f 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Hukumu hiyo dhidi ya Naswiru Mpendekelaki katika kesi ya Rushwa namba 7824/2024 imetolewa chini ya Mhe. Andrew Kabuka, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, Machi 22, 2024.
Kwamba mshtakiwa akiwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kahaazi na mmiliki wa Mpendekelaki Stationary, aliomba na kupokea rushwa ya shilingi 300,000 kutoka kwa *John Bosco Balija* ambaye ni raia wa Uganda ili aweze kumwombea cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA katika mamlaka husika.
Mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na Mahakama.