Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Munde Tambwe akizungumza kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika zahanati ya Bulela iliyopo Manispaa ya Mji wa Geita, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati,Mheshimiwa Stansalaus Mabula na kushoto ni mjumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Daimu Mpakate.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC),Mheshimiwa Stansalau Mabula akizungumza na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika Zahanati ya Bulela iliyopo Manispaa ya Mji wa Geita
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC),Mheshimiwa Stansalau Mabula akiambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua msingi wa uzio wa uwanja wa wa mpira wa miguu Geita katika Halamshauri ya Mji wa Geita wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC),Mheshimiwa Stansalau Mabula akiambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua mradi wa ujenzi wa mpira wa miguu Geita katika Halmshauri ya Mji wa Geita.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikalu (LAAC), wakiongozwa na Makamu mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakonyeshwa mchoro wa ramani ya uwanja wa mpira wa miguu Geita wakati Geita wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo.
………
Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (LAAC) imeagiza watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita kushughulikia changamoto zote zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Geita na kukabidhi taarifa hiyo kwa mkaguzi wa ndani.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Stansalus Mabula wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita.
Alisema changamoto hizo zimesababisha ongezeko la gharama ambazo zimeingiza hasara ya zaidi ya shilingi milioni 480.
“Kamati ya LAAC inakagua thamani ya fedha, katika mradi huu Halmashauri imeingia hasara kwa kuweka kitu ambacho hakiwezi kutumika, Kamati inaona hapa kuna uzembe uliosababisha fedha kupotea,” alisema.
Alisema hasara hizo zimetokana na mambo mbalimbali ikiwemo uwekeji wa nyasi ambazo zinatakiwa zitolewa zote pamoja na kuvunja mkataba na mkandarasi wa awali aliyekuwepo.
“Changamoto hizi zimetokana na kutokuwa na watu wenye weledi na utaalamu pamoja na matatizo ya kiutendeji katika utekelezaji wa mradi huu wakati ulipoanza,” alisema.
Kamati iliagiza watu wote wanaodai fedha zao katika utekelezaji wa mradi huo walipwe fedha zao ikiwemo mzabuni aliyekuwa na kazi kumwagilia nyasi katika uwanja huo na mkandarasi ambaye mkataba wake unavunjwa.
“Na kwenye mpango mpya wa ujenzi wa uwanja lazima kuwe na uwazi, Kamati inatarajia hadi Januari mwaka 2025 uwanja utakuwa umekamilika na kuanza kutumika,” alisema.
Kamati pia ilikagua Jengo la Utawala katika Makao Makuu ya Mji wa Geita na kuridhishwa na utekekelezaji wake.
“Jengo la utawala ni zuri limejengwa vizuri linatoa taswira nzuri kwa Halmashauri, muendelee kulitunza liwe mfano kwa Halmshauri nyingine na muendelee kulitunza ili liweze kutumika kwa miaka mingi zaidi,” alisema.
Kwa upande wa mradi wa Kituo cha Afya katika zahanati ya Bulela katika Halmshauri hiyo, Kamati iliagiza kufanyike marekebisho katika majengo ya kituo hicho ikiwemo milango ambayo haina ubora na sakafu.
“Kamilisheni pia ujenzi wa chumba cha upasuaji ili vifaa viweze kuletwa kwa kuwa huduma hiyo ni muhimu hasa kwa wakina mama wajawazito.
Mheshimiwa Mwenyekiti alitaka mapungufu yote yaliyojitokeza katika mradi huo yatekelezwe ndani ya miezi mitatu na yawasilishwe kwa mkaguzi.