Mwenyekiti wa Bodaboda Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mohamed Iddy akisaini fomu mara baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliofanyika Machi 18, 2024.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa waendesha pikipiki Wilaya ya Nyamagana wakiwa ukumbini kwaajili ya kufanya uchaguzi
……….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mwenyekiti wa bodaboda Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mohamed Iddy ameeleza vipaumbele atakavyo anza navyo mara baada ya kuchaguliwa kwa kishindo na wajumbe wa Mkutano Mkuu.
Uchaguzi huo ulifanyaka Jana Machi 18, 2024 katika ukumbi wa Nyanza uliopo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza.
Alisema kipaumbele chake kwanza ni kutafuta kiwanja cha kujenga ofisi ya umoja wa waendesha pikipiki wa Wilaya hiyo,pili atashirikiana na Jeshi la Polisi na vituo vinavyotoa mafunzo ya udereva kwaajili ya kutoa elimu kwa bodaboda kwani ajali zimekuwa nyingi.
“Kipaumbele changu cha tatu nitashirikiana na viongozi wa Mikoa ili tuweze kupata miradi itakayosaidia chama kujiendesha,pia nitumie fursa hii kutoa rai kwa madereva bodaboda kutii sheria za barabarani ikiwemo kuacha kubeba mishikaki kwani siyo salama kwa afya zenu”, amesema Iddy
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye Barinago amesema wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwaajili ya kuwahimiza bodaboda kuwa wasafi,kuvaa viatu pindi wanapokuwa wanaendesha chombo cha moto,kuwa na lugha zenye staha wakati wote pamoja na kufuata sheria zote za barabarani.
Awali kabla ya uchaguzi mtaalamu wa kupima Ardhi kutoka Ardhi Mtaji Investment Athumani Nasoro, alipata fursa ya kutoa elimu ya masuala ya ardhi kwa waendesha bodaboda.
“kunachangamoto kubwa ya watu wenye kipato cha chini kwenye kumiliki kiwanja ndio maana tumefika hapa kuwapa elimu ya kupata kiwanja kwa kulipia kidogokidogo”, alisema Nasoro
Alisema kunaumuhimu mkubwa sana kuwekeza kwenye ardhi kwani inapanda thamani kila siku na ndio uwekezaji wenye tija.
Alieleza kuwa wana viwanja vya kulipia ndani ya miezi sita,mwaka mmoja na kwa kuanza unalipa robo ya gharama za kiwanja Kishaunaanza kulipia kidogokidogo kila mwisho wa mwezi.
“Endapo mtu atakwama kumaliza kulipia kiwanja kutokana na changamoto mbalimbali Kampuni itakata asilimia 30 na asilimia 70 anarudishiwa muhusika,