Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefika katika Chuo Kikuu cha AgroparisTech kilichopo Paris nchini Ufaransa kwa mualiko maalum ikiwa ni pamoja na kushiriki mahafali ya kuhitimu kwa wataalamu wa Sekta ya Maji kutoka mataifa mbalimbali ambapo sehemu yao ni Kutoka Tanzania wawili wakiwa Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Maji za Lindi na Shinyanga, Mhandisi wa Maji kutola Mamlaka ya Maji Mwanza na Mhandisi wa Maji kutoka Wizarani.
Akizungumza mbele ya wahitimu hao Mhe Aweso amesema kipaumbele cha Wizara ya Maji ni kuendelea kuwajengea uwezo wataalam na watendaji wake ili wawe imara na mahiri kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Watumishi wa Sekta ya Maji katika chuo cha AgroparisTech kupitia ufadhili wa AFD kwa mpango maalum alioanzisha Waziri wa Maji wa kuwajengea watendaji uwezo.
Waziri Aweso ametumia wasaa huu kuomba ufadhili zaidi kwa watumishi wa Sekta ya Maji.
Aidha Mheshimiwa Aweso ametembelea maeneo mbalimbali ya Chuo hiki na kujionea namna gani matumizi ya Teknolojia yanatumika katika kuimarisha sekta ya Maji.
Katika hatua nyingine Mhe Aweso amefanya mazungumzo na uongozi wa Chuo cha AgroParisTech na kutoa wazo la kuanzisha mashirikiano ya kimkakati kati yake na Chuo cha Maji cha Tanzania kilichopo chini ya usimamizi wa Wizara ya Maji.