Katika kuadhimisha wiki ya Maji Duniani Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu limeiasa Jamii kuwa mstari wa mbele kusimamia mpango wa kulinda na kutunza vyanzo vya maji.
Wito huo umetolewa Machi 16,2024 na Meneja idara ya Mazingira Bondi ya maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Paschal Qutaw, kwenye uzinduzi wa wiki ya Maji mjini Morogoro ulioambatana na zoezi la usafi eneo la Mto Kikundi.
Msisitizo uliopo ni jamii kushiriki moja kwa moja katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji, kupunguza athari zitokanazo na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Sophia Mwenda ni Mkuu wa Maabara ya Ubora wa Maji Morogoro amesema athari za uharibifu wa vyanzo vya maji ni pamoja na kupanda Kwa gharama za ankara za maji linalosababishwa na ongezeko la matumizi ya Sawa za kusafisha Maji katika mitambo.
“Nitoe wito Kwa jamii kutunza vyanzo vya maji kwani uharibifu wa vyanzo vya maji unasabisha kupungua Kwa ubora wa Maji hivyo mamlaka zinazosambaza Maji zinatumia gharama kubwa katika kusafisha Maji na kufanya bili za Maji pia kupanda kutokana na kuongezeka Kwa ghalama za uendeshaji”. Amesema Bi Sophia
Kwa ipande wao baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Morogoro wamesema wanatambua umuhimu wa mpango wa kulinda na kutunza vyanzo vya maji unaolenga kunusuru kupanda kwa Ankara za maji na upatikanaji wa maji safi na salama hivyo watashirikiana na mamlaka zinazohusika kilinda vyanzo
Wiki ya maji huadhimisha ifikapo machi 16 hadi 22 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu wa 2024 kitaifa yanafanyika Jijini Dododma na kupabwa na kauli mbiu isemayo “Uhakika wa maji kwa amani na utulivu”.