MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana CCM Taifa UVCCM Rehema Sombi amewasihi vijana wasomi wa wanaotokana na chama cha Mapinduzi CCM kuendelea kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao, kwa kuzingatia kundi hilo kuwa Muhimu kwa maendeleo ya Taifa .
Sombi ameyaeleza machi 16 wakati akifungua mkutano mkuu wa UVCCM vyuo na vyuo vikuu unaofanyika kitaifa mkoani Iringa, ambao umeambatana na uchaguzi wa wajumbe wa Seneti vyuo na vyuo vikuu kitaifa.
Amesema kuwa toka kuanzishwa kwa Seneti ya vyuo na vyuo vikuu Nchini, kundi hili limekuwa ngome ya umoja ndani ya chama cha Mapinduzi CCM, kutokana na umuhimu wake mkubwa wa kujikita katika kuongeza wanachama wapya, kulinda waliopo na kuendelea kufanya tafiti zaidi kwa Nchi nzima idadi ya wapiga kura wanaotokana na wasomi.
Amesema, kutokana na kundi hilo kuwa na tija katika kuchangia ushindi kwa CCM, wanapaswa kuwa tayari wakati wowote watakaohitajika kuhakikisha chama cha Mapinduzi CCM kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu Nchini na uchaguzi mkuu utakaofanyika 2025.
Amesema,hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa miongoni mwa wasomi wachache ndani ya Taifa, ususani katika kutukomboa kwenye mikono ya ukoloni wa utumwa ambao tulikuwa nao awali, hivyo kwa wakati huu ni wajibu wa vijana wasomi kuendelea kuyaishi na kuyaenzi kwa kuungana pamoja kupelekea uongozi wa kifikra na kiuchumi na kuwa sehemu ya Mapinduzi kuanzia ngazi ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Ninawasihi Sana wasomi wenzangu, mara mtakapohitimu mkutano huu na kurudi vyuoni kwenu,nendeni mkakisaidie chama kuhamasisha wanafunzi ili waweze kujiandikisha pia wahamaaisheni wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM”