Na Sophia Kingimali
Chuo cha Bahari Dar es salaam DMI, kwa kushirikiana na Reginal Maritane University Cha nchini Ghana kimeandaa kongamano la tatu la mwaka la kimataifa litakalozungumzia dhana nzima ya uchumi wa buluu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo March 15,2024 jijini Dar es salaam mkuu wa CHUO hicho Dkt Tumaini shaabani Gulumo amesema kongamano hilo,linatarajiwa kufanyika nchini kuanzia July 4 hadi 5,2024, jijini,dar es salaam,katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere (JNICC)huku nchi mbalimbali Duniani zikitarajiwa kushiriki.
“Chuo Chetu kikishirikiana na kile Cha Reginal maritane university Cha nchini Ghana kimeandaa mkutano huo wenye lengo la kutafsiri dhana nzima ya uchumi wa buluu ambapo Tanzania imepewa heshima kubwa ya kuandaa kongamano hili tunajivunia”Amesema Gulumo
Amesema mbali na mambo mengine yatakayojadiliwa kwenye kongamano Hilo ni pamoja na usalama wa bahari ikiwemo uharamia, matumizi mabaya ya baharini ikiwemo uharibifu wa mazingira.
Aidha Dkt, Gulumo ametoa ufafanuzi juu ya dhana nzima ya uchumi wa buluu ikiwemo shughuli nyingi zinazofanyika baharini,ikiwemo sekta ya uchukuzi,uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi, utalii na kilimo Cha mwani na nyinginezo.
Aidha Dr Gulumo Amesema hii ni mara yao ya 3 kuandaa kongamano kama Hilo, wakianzia mwaka 2022 na kusisitiza kuwa kwa sasa wanahitaji utashi wa kisiasa kwani serikali zote mbili zimekuwa zikisisitiza ukuwaji wa uchumi wa buluu ili kutekeleza dhana nzima ya uchumi wa buluu.
Dkt Gulumo ametaja madhumnui makubwa ya kongamano hilo mwaka huu ni kutoa fursa kwa wadau wa uchumi wa buluu kukutana,kujadiliana, na kubadirisha uzoefu ili kukuza uchumui wa buluu.
Dkt, Gulumo ameongeza kuwa DMI ndio Chuo pekee hapa nchini kilichopewa mamlaka kumsimamia mambo yote yanayohusu uchumi wa buluu bila kuangalia vyanzo vingine vya maji vilivyopo nchini.
Sambamba na hayo Gulumo amezitaka sekta mbali mbali kushiriki kongamano hilo, zikiwemo Wizara mbali mbali ambazo zinahusika Moja kwa Moja kwenye sekta ya uchumi wa buluu.
Aidha amezitaja nchi ambazo mpaka sasa zimethibitisha kushiriki kongamano Hilo kuwa ni pamoja na ghana Kenya,Uganda ,korea ambazo zitashiriki mkutano huo huku akitarajia washiriki kuongezeka zaidi kutoa Duniani kote.