UONGOZI wa tarafa ya Pawaga mkoani Iringa imeweka mikakati madhubuti kukabiliana na ukatili wa kijinsia,mimba za utotoni pamoja na maboresho ya sekta ya elimu.
Akizungumza wa mwandishi wetu,Afisa Tarafa, Tarafa ya Pawaga, Emmanuel Ngabuji alisema kuwa kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Tarafa,imeweka mikakati ya kukabiliana na Ukatili WA kijinsia kutoa elimu kwa Kuwafanya Watoto kuwa rafiki wa Karibu wa viongozi ili kuweza kuwa huru kuzungumza yale wanayofanyiwa.
Ngabuji alisema kuwa wamejipanga Kutoa Elimu kupitia Mabonanza ya michezo na Kuwatumia viongozi wa dini,na watu wenye ushawishi kwenye Jamii kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na namna ya kudhibiti mimba za utotoni.
Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari William Lukuvi iliyopo Kata ya Ilolo Mpya kwenye Tarafa ya Pawaga,Aliwasisitiza suala la umuhimu wa Elimu,Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Makuzi. Amewasisitiza Kusoma Kwa bidii ili kufikia malengo Yao,
Aidha Ngabuji aliwaeleza Kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Katika sekta ya Elimu ikiwemo kutoa Fedha ZA miundombinu mbalimbali ya Madarasa,Maabara,Madawati
Alisema kuwa suala la Mimba tunaendelea kutoa Elimu Kwa Wanafunzi kuhusu hatua za ukuaji na mabadiliko ya mwili, kupitia Walimu wa afya na kushirikiana na Maafisa wa afya na Maendeleo ya jamii wanaopatikana katika tarafa ya Pawaga.
Ngabuji alimalizia kwa kusema kuwa tarafa ya Pawaga bila ukatili wa kijinsia pamoja na mimba za utotoni inawezekana kwa kufuata sheria za nchi kwa kuwachukulia hatua wote wanaofanya vitendo hivyo na kuwapeleka kwenye vyombo ulinzi na usalama ili sheria ichukue mkondo wake.