Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewatahadharisha wafanya biashara wanaokiuka maelekezo ya Serikali kwa kuuza Sukari juu ya bei elekezi liyopangwa kutumika kote nchini, ambayo Kilogramu moja ya Sukari ianzie shilingi 2700 na isiyozidi 3200.
Mkuu huyo wa Wilaya amezungumza hayo wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye maduka yaliyopo Same mjini ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza matumizi ya Mashine za kieletroniki wakati wa kutoa risiti kwani kutofanya hivyo ni kosa kisheria na hataua kali zitachukuliwa kwa mfanyabaishara atakaye bainika anakwepa kutumia Mashine hizo.
Baadhi ya wafanyabiashara waliotembelewa na Mkuu huyo wamesema hatua zilizochukuliwa na Serikali juu ya changamoto ya kupanda kwa bei ya Sukari imesaidia kupunguza makali wananchi waliyokuwa wanakabiliana nayo.