Tarehe 06 Machi 2024, Mhe. Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Maputo alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Msumbiji, Mhe. Philip Githiora kwenye Ofisi za Ubalozi zilizopo Jijini Maputo.
Katika mazungumzo yao, Viongozi hao wawili walizungumza masuala ya Ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali. Aidha, walizungumzia masuala yanayohusu Ushirikiano kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kusisitiza haja ya kuimarishwa kwa Jumuiya hiyo kwa maslahi ya Nchi Wanachama
Imetolewa na Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Maputo
12 Machi, 2024.