Mwakilishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Anorld Mapinduzi akikata utepe kuzindua Ofisi mpya za Taasisi inayojihusisha na Maswala ya Mazingira na Uwezeshaji (TEEMO) zilizopo Mikadi katika Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es salaam wakiwemo wadau wa mazingira na Mkurugenzi wa Taasisi ya TEEMO na mshauri wa masuala ya mazingira Winfrida Shonde(wa kwanza kushoto)
Jengo jipya la Ofisi za Taasisi inayojihusisha na Maswala ya Mazingira na Uwezeshaji (TEEMO) zilizopo Mikadi katika Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es salaam ambalo limezinduliwa kwa lengo la kujihusisha na Maswala ya Mazingira na Uwezeshaji.
Mkurugenzi wa Taasisi ya TEEMO na mshauri wa masuala ya mazingira Winfrida Shonde akishiriki katika kupanda Mikoko usafishaji wa mazingira katika Fukwe za Bahari ikiwa ni Moja ya kampeni ya utunzaji wa mazingira.
Picha ya pamoja ya Mwakilishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Anorld Mapinduzi baada ya uzinduzi wa Ofisi mpya za Taasisi inayojihusisha na Maswala ya Mazingira na Uwezeshaji (TEEMO) zilizopo Mikadi katika Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es salaam wakiwemo wadau wa mazingira na Mkurugenzi wa Taasisi ya TEEMO na mshauri wa masuala ya mazingira Winfrida Shonde.
………………..
NA MUSSA KHALID
Serikali imesema itaendelea kushirikiana wa Taasisi inayojihusisha na Maswala ya Mazingira na Uwezeshaji (TEEMO),katika kutoa elimu kwa jamii ili iweze kuyatunza mazingira.
Hayo yamejiri jijini Dar es salaam katika Hafla ya uzinduzi wa Ofisi mpya za Taasisi hiyo zilizopo Wilaya ya Kigamboni ambalo lilitanguliwa na zoezi la usafi katika fukwe za Bahari na upandaji wa mikoko ambapo imewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo NEMC, Ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira na wadau kutoka taasisi mbalimbali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwakilishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Anorld Mapinduzi ameipongeza Taasisi ya TEEMO kwa kuendelea kufanya Jitihada za kuhakikisha mazingira yanalindwa huku akiwataka wadau wengine kuiga mfano huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya TEEMO na mshauri wa masuala ya mazingira Winfrida Shonde amesema kuwa dhamira yao niliendelea kushirikiana na wadau mbalimbali Ili kusaidia kuyatunza na kuhitadhi mazingira katika
Winifrida amesema kuwa wamejipanga kufanya kampeni mbalimbali za kuhamasisha jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira Ili kuepukana na madhara yanayosababisbwa na mabadiliko ya tabia nchi.
“Tunafanya shughuli zetu kwa ajili ya kuwezesha jamii Kufahamu namna ya kutoa kipaumbele katika utunzaji wa mazingira”Amesema Winfrida
Aidha amesema jamii na wadau mbalimbali wamekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia kuhakikisha wanafikisha ajenda ya mazingira Mbele.
Katika Hatua nyingine amesema wametumia siku ya Wanawake Duniani kushiriki kufanya usafi katika fukwe za Bahari na upandaji wa mikoko ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira.