RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 8-3-2024, kwa ajili ya kuufunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola , uliofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi ya kumpongeza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe.Patricia Scotland, wakati akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola, kabla ya kufungwa mkutano huo leo 8-3-2024, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar.(Picha na Ikulu).
WASHIRIKI wa Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufunga mkutano huo, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 8-3-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufunga mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 8-3-2024.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Sanduki cha Njumu (Kasha) Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, baada ya kumaliza kuhutubia na kuufunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 8-3-2024.(Picha na Ikulu).