Abiria wa meli ya MV Cralias inayofanya safari kati ya Mwanza na Ukerewe na mkazi wa Musoma Bw. Michael Selemani akifanya mahojiano na mwandishi wa TBC Khalid Gangana kabla ya meli ya MV Cralias kuondoka katika bandari ya Mwanza Kaskazini.
…………………………………………………………
Wataalamu wa masuala ya usalama katika bandari za Ziwa Victoria mkoani Mwanza kwa sasa wanajitahidi kuchukua hatua mbaimbali za kiusalama kenye usafiri wa majini jambo amabalo limesaidia wasafiri wanaotumia vyombo vya majini katika ziwa hilo kutambua na kuelewa masuala mbalimbali muhimu kwa usalama.
Hayo yamesemwa leo na Bw.Michael Selemani mkazi wa Musoma na mfanyabiashara anayetumia usafiri wa meli katika ziwa Victoria leo akisafiri na meli ya MV Cralias kutoka Mwanza kuelekea Ukerewe.
Michael Selemani anasema kabla ya safari wamekuwa wakitagaziwa na maofisa wa meli taratibu zote za kiusalama jambo ambalo kipindi cha nyuma lilikuwa halifanyiki mara kwa mara hivyo kuwapa abiria ufahamu wa masuala ya kiusalama kabla ya kuanza safari.
Michael amewashauri abiria wanaotumia vyombo vya majini kutotumia pombe kabla ya safari kwa sababu ukilewa pombe niwazi ikitokea dharura yoyote majini hauwezi kujiokoa au kukumbuka masuala ya kiusalama ili kujiokoa katika misukosuko mara inapotokea ajali majini.
Michael amewashukuru wafanyakazi wa mamlaka ya Bandari (TPA) mkoani Mwanza kwa kazi wanayofanya ya kuhakikisha wakati wote wanakuwa makini na masuala ya usalama majini wakati wa safari na kuwakumbusha abiria mambo muhimu ya kuzingatia kiusalama wawapo safarini.
Kabla hatujaanza safari kutoka Mwanza kuelekea Ukerewe au kutoka Ukerewe kwenda Mwanza maofisa wa TPA wanatutangazia na kutuelezea mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya safari tena kwa lugha zaidi ya tatu ambazo ni Kiswahili, Kiingereza na lugha za makabila ya kule visiwani ikiwemo Kikerewe na maeneo mengine.
Meli ya MV Cralias ikiondoka katika bandari ya Mwanza kaskazini kuelekea Ukerewe.
Abiria wanaosafiri kwenda kisiwa cha Ukerewe wakielekea kupanda Meli ya Mv Cralias katika bandari ya Mwanza Kaskazini ili kupanda meli.
Abiria wanaosafiri kwenda kisiwa cha Ukerewe wakielekea kupanda Meli ya Mv Cralias katika bandari ya Mwanza Kaskazini ili kupanda meli.