Tanzania inashiriki katika Mkutano wa wa siku mbili wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaohusu Ubajilishanaji wa Taarifa Binafsi kwa nchi hizo unaofanyika jijini Kampala. (East Africas Data Exchange Forum).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taarifa Binafsi Bwana Emmanuel Mkilia ametoa taarifa ya hali ilivyo hadi sasa kwa upande wa Tanzania na kuzitaka nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki kuwa na Mfumo mahususi wa utekelezaji wa Matakwa ya makubaliano ya Afrika (Mkataba wa Malabo) na ule wa nchi za Afrika Mashariki.
Alisisitiza kuwa Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Tanzania ni kutokana na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ahadi ya Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 ya CCM ambayo inawahakikishia wananchi kuwa taarifa zao Binafsi na faragha zitalindwa ikiwa ni moja pia ya utekelezaji wa Haki za Binadamu kwa watanzania.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Tume Bwana Mkilia pamoja na ujumbe wake wamtemtembelea Balozi wa Tanzania anayewakilisha Tanzania nchini Uganda Mhe. Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli.
Hali kadhalika Bwana Mkilia amefanya mazungumzo na Wakuu wenzake wa Tume za Ulinzi wa Taarifa Binafsi za nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki.