RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar ,kuhudhuria kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo 5-3-2024.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI wa Dini,Wananchi na Viongozi Wastaafu wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika kisomo cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 5-3-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi wa Serikali,Masheikh na Wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi,katika kisomo cha Hitma na Dua, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, Jijini Zanzibar, iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo 5-3-2024.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Zanzibar na kutoka nje ya Zanzibar wakijumuika katika Kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 5-3-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na kutoka shukrani kwa Wananchi, baada ya kumalizika kwa Kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Masjid Jamiu Zinjbar Mazizini Wilaya ya Magharibu “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 5-3-2024.(Picha na Ikulu)
…………………………
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametaja baadhi ya mambo aliyojifunza kutoka kwa Hayati Mzee Mwinyi wakati wa uhai wake.
Hayati Mzee Mwinyi alikuwa na Subira kubwa wakati alipokuwa kiongozi hususan kipindi cha mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi. Watu walimsema vibaya kwa mambo ya kutunga katika vyombo vya Habari lakini hakuwahi kumjibu yeyote kwa mabaya waliyomsema.
Alhaj. Dk. Mwinyi aliongeza na kusema yeye amejifunza kusubiri kwa fundisho alilolipata kwa Mzee wake kwa kumpa mafunzo mema.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema wakati Marehemu baba yake alipokuwa akitibiwa Uingereza aliwataka madaktari na familia arudishwe nyumbani na baadae apelekwe Zanzibar, maneno hayo aliyarudiarudia hata baada ya kufika Dar es Salaam.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika Dua ya khitma iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambayo imefanyika leo tarehe: 05 Machi 2024, Msikiti wa Zinjibar Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Rais Dk. Mwinyi ameishukuru kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mazishi inayoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na wajumbe wake.