Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiango Kilonzo akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotangaza kuanza kwa kampeni ya kuhakikisha filamu na nyimbo zinazotumika kwenye vyombo vya usafiri hasa mabasi zinafuata maadili sheria na kanuni zilizowekwa nchini kulia ni Cralence Chelesi Afisa Maendeleo wa Filamu na kushoto ni Evordy Kyando Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiango Kilonzo wakati alipokuwa akizungumza nao.
Evordy Kyando Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akisistiza jambo katika mkutano huo kutoka kushoto ni Cralence Chelesi Afisa Maendeleo wa Filamu Bodi ya Filamu na katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiango Kilonzo.
…………………………………………………..
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiango Kilonzo, amesema atawatuma maafisa wake kukamata madereva wanaoonyesha filamu na miziki kupitia mabasi ya mikoani kuonyesha picha na video jongevu zisizo na mahadili wala kibali kutoka bodi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kilonzo alisema kuwa wamiliki na waendeshaji wa mabasi wanatakiwa kuwa makini na filamu na miziki wanayopiga katika vyombo vyao.
“Kazi yoyote yenye mambo ya kijambazi, ngono na kitendo cha utekaji nyara utakaoleta ugaidi baina ya nchi na nchi haziruhusiwi”
“Kuanzia sasa nitatuma maofisa wangu watakuwa wanasafiri na mabasi bila kujitambulisha ili kuangalia kama sheria inafatwa au haifatwi na kuonyesha filamu au miziki hisiyo na maadili kwa kuwa tumeshaongea sana”
“Kanuni na sheria zipo wazi na tumekuwa tukiwakumbusha mara kwa mara lakini wamekuwa wakivunja sheria ya mwaka 2014 kwa kuonyesha kitu ambacho hakina maadili ya kitanzania unatakiwa kuonyesha kazi zenye kibali cha bodi ya filamu” alisema Kilonzo
Kwa upande wake Mwanasheria Evordy Kyndo alisema kuwa sheria itafatwa kwa mmiliki na dereva wa chombo husika kaekutwa na makosa hayo.