……………………..
Arusha .Nchi ya Somalia imejiunga Rasmi kuwa mwanachama wa nane wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika makao Makuu ya EAC Jijini Arusha.
Ambapo kujiunga kwake kuwa mwanachama itasaidia suala Zima la msukumo wa changamoto za ajira kwa nchi wanachama pamoja na kupanua wigo mpana wa soko la pamoja .
Aidha Kujiunga kwa Somalia ni kutokana na kikao cha Wakuu wa nchi kilichoketi desemba 25 mwaka Jana jijini Arusha,kukubali Nchi hiyo kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt.Peter Mathuki katika sherehe fupi ya kupandisha bendera na kupokea hati za uanachama wa Somalia makao makuu ya EAC Jijini Arusha amesema soka la Jumuiya limepanua wigo na kuwa na watu takribani milioni 350 kwa Sasa na hivyo kuiwezesha jumuiya hiyo kujipanua kibiashara.
Aidha Dkt.Mathuki amesema kuwa kuongezeka kwa soko hilo la watu wanaofikia milioni 350 kutaondoa changamoto za upungufu wa ajira na kupelekea wananchi kuchangamkia uzalishaji wa bidhaa na kuuza katika soko la pamoja.
Naye Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweso amesema wanayo furaha kubwa kukamilisha safari ndefu ya miaka 12 na safari hiyo ilikuwa na Kazi Kubwa ya changamoto lakini hawakuchoka kufikia hatua hiyo ya kukamilisha utaratibu wa mwisho wa kujiunga na EAC.
Amesema Jumuiya hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Somalia na nchi zote wanachama kwa kuwa nchi ya nane kujiunga na Jumuiya hii na tunaleta mchango Mkubwa tutakaotoa kuleta maendeleo ndani ya nchi zetu katika uchumi biashara n.k.
Ameeleza kwamba changamoto zipo ndani ya Somalia tunaendelea kuzifanyiakazi na Kwa mwaka uliopita Kuna mambo mengi tulioyafanya kuhakikisha tunawapa Picha nzuri wanachama wengine kukiwa na wanachama zaidi ya 350.
Awali Waziri wa viwanda na biashara wa Somalia,Jibril Abdirashid Haji Abdi amesema wanaendelea na wanayofuraha kuwa sehemu ya nchi nane za Jumuiya hiyo ya EAC na wanashukuru kwa kukaribishwa Rasmi na kuahidi kushirikiana na nchi zengine za Jumuiya hiyo kukuza uchumi.