Dar es Salaam, Tanzania, Februari 29,2024
Samsung Electronics kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuendelea kutawala katika soko la kimataifa la kuuza televisheni duniani, kwa kufanikiwa kuongoza kuteka masoko mfululizo kwa miaka 18 katika katika tasnia hii.
Kampuni ya utafiti wa masoko ya Omdia imebainisha kuwa Samsung imetawala kwa asilimia 30.1% soko la kimataifa la TV mwaka wa 2023, na hivyo kuendeeleza hadhi yake kama kiongozi wa sekta hiyo tangu 2006. Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa kimkakati wa kampuni katika kategoria za runinga za ubora na skrini kubwa, za modeli ya kisasa inatotumia teknolojia za QLED na OLED.
Tangu kuzinduliwa kwake mwaka wa 2017, safu ya runinga za QLED za Samsung, pamoja na miundo ya hivi punde ya Neo QLED, imevuka mauzo ya jumla ya kufikia runinga milioni 40. Mnamo 2023 pekee, safu ya QLED ilipata mauzo ya runinga milioni 8.31. Wakenya wanafurahia ubora wa picha usio na kifani na ubora wa sauti wa runinga aina ya Neo QLED iliyozinduliwa nchini humo mwaka wa 2022.
Manish Jangra, Mtendaji Mkuu wa Tanzania, Samsung Electronics East Africa Ltd alisema: “Tunaposherehekea mfululizo wa miaka 18 wa Samsung kama kiongozi wa soko la TV duniani, ninajivunia kuwa sehemu ya timu inayovuka mipaka mara kwa mara. Kujitolea kwetu kwa miundo ya kisasa ya QLED na OLED kumekuwa muhimu katika kudumisha msimamo wetu usio na kifani. Tunatazamia kuwapatia uzoefu wa kipekee zaidi kwa wateja wetu.”
Samsung imedai inaongoza katika sekta ya mauzo ya Televisheni – haswa kwa TV zenye skirini zaidi ya inchi 75 na bei yake ni zaidi ya $2,500 (Takriban Tzs6.4 milioni). Kampuni imerekodi kuteka soko kwa asilimia 60.5% katika mauzo ya TV za bei ya zaidi ya $2,500, huku pia ikiendelea kuongoza kwa asilimia 33.9% ya mauzo ya TV zenye ukubwa wa zaidi ya inchi 75 . Zaidi ya hayo, kutokana na mauzo thabiti ya miundo ya inchi 98, TV za zaidi ya inchi 90 zimeendelea kutawala soko kwa asilimia 30.4%.
kutawala katika soko la kimataifa la kuuza televisheni duniani, kwa kufanikiwa kuongoza kuteka masoko mfululizo kwa miaka 18 katika katika tasnia hii.