Happy Lazaro,Arusha .
Arusha.Mamia ya Wananchi wamejitokeza kuiaga miili ya watu 25 waolifariki katika Ajali ya gari iliyotokea mnamo tarehe 24 febuari katika barabara ya Ngaramtoni namanga Arusha .
Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt Pindi Chana akizungumza katika uwanja wa mpira Stadium jijini Arusha amesema Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia Suluhu Hassan alihimiza zoezi hilo liratibiwe na kuhakikisha majeruhi waliopo hospitali wanapata matibabu .
Aidha amesema kama Serikali wataendelea kuwa pamoja na familia hizo kwa ajili ya kuwapumzisha ndugu hao kwani wameacha pengo kubwa kwao na kwa serikali.
“ni pigo kubwa kwa mkoa wa Arusha na kwa Taifa kwa ujumla kwani msiba huu ni wa kwetu sote na hatuna budi kuungana na kuendelea kumwomba Mungu azidi kutuepusha na majanga mbalimbali “amesema.
Hata hivyo ametaka vyombo husika kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaokiuka sheria za usalama barabarani ili matukio hayo yasiweze kujirudia na kusababisha masafa kama hayo tena.
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela amesema kuwa wameweza kusikiliza maelekezo yote yaliyotolewa na Rais ambayo alielekeza kuhakikisha majeruhi wote wanapata huduma ikiwemo kuwashika mkono ndugu wa waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Baadhi ya viongozi wa dini na wananchi walishauri kufanyika ukaguzi wa magari mara kwa mara ili kuepusha ama kusababisha Ajali za mara kwa mara.
Hata hivyo miili hiyo itasafirishwa kwa ajili ya kwenda kupumzishwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha,na wengine Saba kutoka mataifa ya nje.