Zaidi ya wananchi ELFU TANO wa mkoa wa KASKAZINI UNGUJA wanatarajiwa kufikiwa na huduma ya kambi ya matibabu mwanzoni mwa mwezi machi.
Wakizungumzia kambi hiyo ya afya bora maisha bora ya taasisi ya maisha bora Zanzibar– ZMBF. Afisa mtendaji mkuu wa taasisi hiyo FATMA FUNGO na Mkurugenzi kinga na elimu ya afya wa wizara ya afya Zanzibar DKT . Salim SLIM wamesema huduma hiyo itatolewa kwa wananchi na madaktari bingwa Kuanzia machi 5 hadi 8.
Mkuu wa wilaya ya KASKAZINI A, Othman Ali Maulid amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma hiyo ya afya bure ambayo inadhaminiwa na Benki ya watu wa Zanzibar.
Wameeleza uchunguzi na matibabu ya maradhi mbalimbali utafanyika katika kambi hiyo ukiwepo kupima damu, saratani ya matiti, tezi dume pamoja na lishe Kwa watoto.
Meneja masoko wa PBZ,
SEIF SULEIMAN MOHAMMED Amesema udhanimi huo ni sehemu ya faida ya Benki hiyo ambayo inarudishwa Kwa jamii.
Kambi ya Afya Bora Maisha Bora inayo simamiwa na taasisi ya Zanzibar maisha Bora – ZMBF ambayo mwenyekiti wake ni mke wa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi Inatarajia kufanya kambia kama hizo za matibabu Kwa mikoa yote ya Unguja na Pemba.