Na Eleuteri Mangi, WANMM
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amemkabidhi Msanii wa.kizazi kipya Nasibu Abdul (Diamond Platnum) hati za umiliki wa viwanja vitatu ananvyomiliki katika maeneo mbalimbali katika jijini Dar es salaam.
Makabidhiano hayo yamefanyika viwanja vya shule ya Msingi Bunju A Februari 22, 2024 jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi hati hizo Waziri Silaa amewahamasisha wananchi maeneo mbalimbali nchini kujitokeza kumilikisha viwanja vyao kwa kufuata mchakato wa utoaji hati hadi kukabidhiwa hati zao.
Kwa upande wake Msanii Diamond ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na ubunifu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuja na wazo la Kliniki ya Ardhi ambayo inawasaidia watu kupata hati zao kwa muda mfupi tofauti na mchakato wa awali ambao ulikuwa unatumia muda mrefu zaidi kupata hati.
Aidha, Msanii Diamond amewasihi wasanii nchini, watumie fursa inayotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Kliniki ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini ili wapate hati za viwanja vyao wavitumie kama rasilimali zao kukuza uchumi wao.
Zoezi la Kliniki ya Ardhi linaloendelea jijini Dar es salaam limeanza Februari 19-28, 2024 wilaya ya Kinondoni katika mkoa wa Dar es salaam Dar es salaam.