Benki ya NMB imetunukiwa Tuzo ya Benki Bora ya Biashara Ndogo na za Kati Tanzania kutoka Jarida la Kimataifa la Global Finance katika hafla iliyofanyika jijini London, Uingereza leo.
Mchakato wa kupata washindi wa Tuzo hizo za Benki Bora za Biashara kwa mwaka 2024 ulihusisha tathmini ya kina ya mawasilisho na tafiti huru, pamoja na maoni kutoka kwa wataalamu wa kisekta na wabobezi wa masuala ya biashara na teknolojia duniani.
Pamoja na mambo mengine, tuzo hii imetambua mchango wa Benki ya NMB katika kuwawezesha wajasiriamali nchini kukuza biashara zao kwa:
Kuwapa mikopo yenye riba nafuu kwa wakati ikiwemo mikopo kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake au ambazo huduma zake zinamgusa mwanamke, kupitia Hati Fungani ya Jasiri.
Kuwapa elimu ya fedha kuhusu ukuzaji wa biashara zao kupitia majukwaa ya NMB ya Business Clubs, Business Executive Network na mengine mengi.
Uwekezaji katika mifumo ya teknolojia inayowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi na haraka kwa njia za kidijitali ikiwemo NMB Mkononi, NMB Direct, mikopo ya kidijitali isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta), na huduma nyingine nyingi.
Tuzo hii imetolewa na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Uhariri wa Jarida la Global Finance – Bw. Joseph Giarraputo na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Biashara NMB – Bw. Alex Mgeni, alieambatana na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Tunawashukuru wateja na wadau wetu kwa kutuchagua kama mshirika wa kuendeleza biashara zao!