Mkuu wa kitengo Cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad akiwa sambamba na wananchi na viongozi wa Serikali ya Mtaa katika zoezi la ufanyaji wa usafi katika Mtaa wa midizini Kata ya Manzese Manispaa ya Ubungo ambao umefanyika Leo Feb 17,2024 katika Manispaa hiyo.
Mkuu wa kitengo Cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad akionyesha kwa vitendo ushiriki wake katika zoezi la usafi katika Mtaa wa midizini Kata ya Manzese Manispaa ya Ubungo ambao umefanyika Leo Feb 17,2024 katika Manispaa hiyo.
Balozi wa Mazingira Manispaa ya Ubungo Lulu Sadru Sengulo akishiriki kwa vitendo katika zoezi la ufanyaji wa usafi katika Mtaa wa midizini Kata ya Manzese Manispaa ya Ubungo ambao umefanyika Leo Feb 17,2024 katika Manispaa hiyo.Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa midizini Kata ya Manzese Manispaa ya Ubungo wakiwa wameshiriki kwenye zoezi la usafi ikiwa ni baada ya Mtaa huo kuwa wa mwisho katika kampeni ya usafi ya KAU-SAPEU (Kataa Uchafu, Safisha, Pendezesha Ubungo) na kupewa bendera ya balozi wa Uchafu Ubungo.
…………,……….
Wakazi wa Mtaa wa midizini Kata ya Manzese Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam wamewasisitiza kuhakikisha wanafanya usafi kwenye maeneo yao ikiwemo mitaro yote inayowazunguka kusafishwa mara kwa mara hasa kwa kuacha kutiririsha maji machafu katika mitaro.
Kauli hiyo imekuja kufuatia wakazi leo wakiongozwa na viongozi wa Serikali ya Mtaa huo kuingia mtaani kufanya usafi, ikiwa ni baada ya Mtaa huo kuwa wa mwisho katika kampeni ya usafi ya KAU-SAPEU (Kataa Uchafu, Safisha, Pendezesha Ubungo) na kupewa bendera ya balozi wa Uchafu Ubungo.
Akizungumza na wakazi wa Mtaa huo Mkuu wa kitengo Cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad ambapo amesema kuwa huo utakuwa ni muendelezo kwani atakuwa akipita mara kwa mara ili kuangalia kama usafi unaendelea kufanyika.
Lawi amewataka wananchi kuchangia fedha za kubeba taka na kuwataka kutambua usafi ni jukumu la kila mmoja katika Mtaa wake na dhumuni ni kuweka mazingira yaliyozunguka kuwa safi na salama
Katika zoezi hilo ufanyaji wa usafi pia wameshiriki mabalozi wa Mazingira akiwemo Lulu Sadru Sengulo ambapo amewahamasisha wananchi kupenda kufanya usafi kwenye maeneo yao.
Ikumbukwe kuwa, kampeni hiyo ni endelevu na kila baada ya miezi mitatu mshindi atatangazwa na Mtaa utakao kuwa wa mwisho utapata bendera ya Balozi wa Uchafu Ubungo.