Na Sophia Kingimali
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk.Alex Malasusa amewasihi wachungaji kutopokea miili ya watu waliofariki ambao hawakuwa wakihudhuria ibada kanisani wakati wa uhai wao kwani kufanya hivyo ni kuukosea mwili huo.
Hayo ameyasema leo Februari 14,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa ibada maalumu ya kuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa aliyefariki Februari 10 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI)iliyofanyika katika Ushiriki wa Azania Front kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali.
Amesema Lowassa alikuwa mpenda ibada wakati alipokuwa na uwezo wa kwenda kanisani alifanya hivyo kila wakati hivyo hivyo nitoe rai kwa wananchi wote bila kujali dini zao kutumia nyakati kama hizi kumtafakari Mungu zaidi na kujisogeza karibu na Mungu.
“Ukileta mwili kanisani wakati mhusika alipokuwa hai alikuwa na uwezo wa kukubali au kukataa kuhudhuria ibada ni kuuonea mwili huo, “amesema Dk. Malasusa.
Amesema Edward alipenda ibada enzi za uhai wake ambapo hata wachunga waliongoza ibada hapa kanisa wataongea alikuwa mtu wa ibada.
Dk. Malasusa ukweli utabaki kuwa ukweli haijalishi wanasema nini watoto na Mke wa Lowassa hongereni kwa kuwa na Baba ambae kila mtu anasema mazuri yake na amegusa maisha ya waliowengi.
“Kama hujawah kupotelewa na ndugu mzazi huwezi kuelewaa neno pole ulikuwa unacheka nae mnashare lakini leo hayupo jambo kubwa ni kumuomba Mungu akuondolee maumivu na kukutia nguvu,”amesema.
Amesema wao wanaomwamini Mungu duniani wqnapita baada ya maisha hayo kuna maisha mengine.
“Edward anastahili makofi kweli kweli alipenda ibada na mshukuru mama Regna alikuwa bega kwa bega pamoja kuwa ni mkatoliki kweli kweli lakini walihimizana kwenda ibada Mama Regna na familia kwa ujumla niwaombe yale yote mliyotenda wakati wa uhai wa Edward Lowassa naomba myaendeleze,” ameongeza.
Aidha amesema hakuna ulazima katika kanisa kufungua na kuona mwili wa mwanadamu aliyefariki na sio sheria ya makanisa au maandiko ya bibilia kufanya hivyo.
“Tuwe tunatazamana tukiwa hai tusisubiri mtu amelala msifikirie kwenda kuaga ni lazima ufungue mtu umwone siyo lazima naiopongeza familia ya Lowassa kwa kufanya hivyo na ikawe mfano kwa wengine,” amesema.
Naye Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni amesema Waziri Mkuu Mstaafu Lowassa angeweza kuishi zaidi kama isengekuwa ajali mbalimbali za kisiasa alizokutana nazo.
Ameeleza kuwa siasa ilimletea mgogoro mkubwa lakini alisimama na kuacha alama na siku zote alikuwa mtu mwenye upendo.
Amesema 2015 walianza safari ya matumaini ambayo kote walipokwenda watanzania walionyesha matumaini makubwa kwa sababu waliamuamini sana Lowassa kwamba ndiye kiongozi anayeweza kuwavusha watanzania katika harakati za kuwaongoza
“Tunahitaji wazee kama mzee JajiJoseph Warioba amemuelezea Lowassa mwanzo mwisho uliongea kutoka moyoni hukuongea kama mwanasiasa Lowassa aliikuwa mvumilivu, “amesema Dk. Chegeni.
Kwa upande wake Mtoto Lowassa Fredrick Lowassa amesema muda wote alipokuwa na nguvu alikuja kanisa na amewafundishwa hivyo.
“Hata tulipokuwa hatujaenda kanisa kuna jicho baba alikuwa anakuangalia unajua una Kosa hadi leo ametufundisha kupenda ibada,”amesema Fredrick.
Amewashukuru viongozi wote na wananchi wote walikuwa wanamuombea baba yao wakati akiuugua na kesho Monduli watakuwa na ibada ya kuomboleza.
Waziri Mkuu Mstaafu Hayati, Edward Lowassa anatarijia kuzikwa Februari 17 mwaka huu Ngarash Wilaya ya Monduli.