Kufuatia soko mazao ya nyuki hususani asali kukua kwa kasi ulimweni na kubadili maisha ya wafugaji kiuchumi,Muungano wa wakulima wa Miti Tanzania TTGAU kwa kushirikana na shirika la chakula duniani FAO uko mbioni kuanza ujenzi wa kituo cha Kukusanya na Kuchakata mazao ya nyuki katika kijiji cha Ninga wilayani Njombe ambacho kitagharimu zaidi ya mil 89 hadi kukamilika kwake.
Katika mkutano uliyokutanisha wadau wote waliyokwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya Nyuki wenye lengo la kutazama fursa za masoko,changamoto na mikakati ya kukuza kilimo hicho,Mkurugenzi wa Muungano wa Wakulima wa Miti Tanzania (TTGAU) Castory Timbula na shirika la FAO limeona upotevu wa mazao ya nyuki hususani asali wakati wa mavuno na kisha kuanza mchakato wa ujenzi wa kituo cha kuongeza thamani mazao ya nyuki jambo litakalo ongeza pia fursa za ajira kwa vijana na masoko ya uhakika.
Timbula amesema licha ya jitihada za wadau na serikali kuendelea kuboresha sekta ya nyuki na mazao ya misitu lakini elimu ya ufugaji wa kisasa imeendelea kutolewa kwa wakulima na wafugaji ili kuzalisha mazao bora na kisha kusema kwamba katika mkutano huo uliyokutanisha wafugaji ,wasambazaji wa vifaa vya ufugaji nyuki,wafanyabiashara wa mazao ya nyuki na maofisa wa serikali wanakwenda kutoka majibu ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta hiyo na mikakati ya kulifikia soko la uhakika.
“Hapa leo tumekutana wadau wote weliyopo kwenye mnyonroro wa thamani wa mazao ya misitu na nyuki kwa lengo la kuangalia changamoto na mikakati ya kulifikia soko na kwamba hatua hiyo imekuja kutokana na Njombe kuwa na mwamko mdogo wa ufugaji wa nyuki licha ya kuwa na mazingira rafiku ya kilimo cha Nyuki,alisema Tumbula”
Akieleza kuhusu ubora wa mazao ya nyuki na hali ya uzalishaji wa malighafi hiyo Daudi Kumbulu ambaye ni afisa nyuki mkoa wa Njombe anasema licha ya kuwa ya Njombe kuwa na mazingira rafiki kwa ufugaji wa Nyuki lakini bado mwamko wa wau haurizishi kwasababu hadi sasa kuna mizinga zaidi ya elfu 40 huku pia akisema kwa mwaka 2023 tani zaidi ya 200 za asali zilivunwa hivyo jamii inapaswa kuchangamkia fursa hiyo.
Wakati wadau na serikali ikihamasisha jamii kujitokeza kuwekeza katika sekta ya nyuki ,wakulima wa miti na wafugaji wa Nyuki akiwemo Albano Mlowe wanassema kikwazo kikubwa kwao ni soko kwasababu hata wachache walio anza kufuga hawana soko la uhakika huku pia wakisema kujengwa kwa kituo cha kuchakata mazao ya mazao ya nyuki kutakwenda kuwa muarobaini kwao
“Tunaipongeza serikali kwasasa inafanya kila jitihada za kuendeleza sekta mbalimbali hususani sekta ya Nyuki lakini tuombe masoko ya uhakika ili kuhamasisha watu kufuga nyuki,alisema Mlowe”