Na.Abel Paul,Jeshi la Polisi-Arusha
Jeshi la Polisi Katika kuhakikisha linaendelea na ulinzi wa raia na mali zao hapa nchini kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini (STPU) kimeshiriki katika kampeni ya upandaji miti zaidi ya elfu moja katika kata ya monduli Juu Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha ambayo ilizinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura.
Akiongea mara baada ya zoezi la upandaji miti Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo wa mifugo nchini Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema kikosi hicho kimeshiriki zoezi la upandaji miti pamoja na wananchi ili kuhakiksha mazingira yanabaki salama.
Ameongeza kuwa anatambua kuwa Jamii hiyo ni kifugaji ambapo amewaomba kuweka jitihada katika kutunza mazingira ili wawe salama Pamoja na mifugo yao huku akiwaomba wafugaji wengine nchi nzima kushiriki vyema katika kupanda miti kwenye maeneo yao.
Sambamba na hilo kamanda Pasua amewaomba wananchi kuendelea kutoa taatifa za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo hapa nchini huku akitoa wito kwa wafugaji kufuata sheria nataratibu za usafirishaji wa mifugo nje ya nchi huku akibainsha kuwa watao kiuka wataendelea kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Monduli Juu Mheshimiwa Thomas Meiyan amesema kuwa wananchi wa Monduli wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu hassan kwa namna alivyo toa fedha nyingi katika miradi ya maendeleo ya kata ya Monduli juu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Emairete Upendo Machanja licha ya kupongeza Jeshi la Polisi amesema miti hiyo itakuwa chachu ya ufaulu na maendeleo ya kitaaluma kwa ujumla ambapo amesema kuwa shule hiyo ilikuwa na uwazi ambao unakwenda kuisha baada ya miti hiyo kustawi.
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Zawadi Kituya amesema miti hiyo itabadilisha mwonekano wa shule yao huku akibainisha kuwa wataitunza vizuri ili iwasaidie kitaaluma.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Emairete kata ya Monduli juu Mboyo Kaileza amesema wao kama wafugaji tayari wameshauriana kutoingiza mifugo yao katika eneo hilo ambalo limepandwa miti zaidi ya elfu moja katika hiyo nae neo la shule ya msingi Emairete.