Na. Beatus Maganja.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imeendelea kupokea watalii kutoka Mataifa mbalimbali katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara ambapo Februari 5, 2024 imepokea jumla ya watalii 125 ikiwa ni baada ya kupokea kundi la kwanza lenye idadi ya watalii 102 kutoka Uingereza Februari 03,2024
.Imetajwa kuwa watalii hao watoka katika Mataifa ya Austria, Ubeligiji, Canada, Denmark, Ecuador, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Korea.
Huku wengine wakitokea Mataifa ya Luxembourg, Urusi, Norway, Ureno, Singapore, Hispania, Uingereza na Marekani.
Meli ya Le Champlain ya Kampuni ya The Hebridean Sky kutoka ufaransa ndiyo iliyobeba watalii hao na kuwafikisha katika hifadhi hiyo kongwe Duniani kwa ajili ya shughuli za utalii.
Ikumbukwe kuwa mafanikio yote yanayoonekana leo ni matokeo ya jitihada za dhati za kuchechemua utalii wa nchi yetu zilizofanywa na Muongoza watalii namba moja Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipocheza Ile Filamu Maarufu ijulikanayo kwa jina la Tanzania The Royal Tour.