Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Cyriacus Binamungu, Mshauri wa Wanafunzi na Mratibu wa Michezo Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Zitta Mnyanyi pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja katika kilele cha Mlima wa Pugu wakati wakishiriki Bonanza la michezo lililofanyika February 3, 2024 katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Kaimu Naibu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo hicho katika kilele cha Mlima wa Pugu wakati wakishiriki Bonanza la michezo lililofanyika February 3, 2024 katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Cyriacus Binamungu (wa kwanza kushoto), Kaimu Naibu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba, wakiwa pamoja na Muongoza Watalii, Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi Bw. Joseph Jabir (kwanza kulia) wakati akiwaongoza wafanyakazi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Cyriacus Binamungu akizungumza jambo wakati akifungua Bonanza la michezo lililofanyika February 3, 2024 katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Cyriacus Binamungu akiwa na Wafanyakazi wa chuo hicho wakipanda kilele cha Mlima Pugu wakati washiriki bonanza la Michezo lililofanyika February 3, 2024 katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakishiki Michezo mbalimbali katika Bonanza lililofanyika February 3, 2024 katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani (Picha na Noel Rukanuga)
……………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wameshiriki katika Bonanza la michezo, lililoandaliwa na Kitengo cha Huduma za Wanafunzi kwa lengo la kuimarisha afya, kuendeleza utamaduni wa kupenda michezo na kuongeza ufanisi kazini, wakiwa katika umoja na mshikamano zaidi ili kuleta tija kwa Taifa.
Bonanza hilo limefanyika February 3, 2024 katika Kituo cha Utalii cha Pugu Kazimzumbwi (Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi) uliopo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, ambapo wafanyakazi hao wamepata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo matembezi ya kupanda mlima wa Pugu uliopo katika Msitu huo, kuruka kamba, draft, bao, karata, kuangalia vituo vya utalii kama vile Bwawa la Minaki, Panzi Tanzania, Pango na michezo ya kutumia ubunifu.
Akizungumza wakati akifungua Bonanza hilo Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Prof. Cyriacus Binamungu, amesema kuwa lengo la Bonanza ambalo limewakutanisha pamoja waalimu na wafanyakazi waendeshaji (Academic & Administrative Staff) kwa ajili ya kuimarisha afya, umoja na mshikamano.
Prof. Binamungu ameongeza kwa amesema Bonanza hilo ni sehemu ya mkakati wa Chuo Kikuu Mzumbe wa kuendeleza Taasisi ili kuleta tija kwa jamii.
“Mkiwa na afya njema, mshikamano na maelewano; utendaji wa kazi wa pamoja utafanyika vizuri na kuleta manufaa yenye tija kwa Taifa” amesema Profesa Binamungu.
Amefafanua kuwa Bonanza hilo wamelitumia kama sehemu ya kufanya mazoezi pamoja na kushiriki chakula na vinywaji kwa pamoja jambo ambalo limeleta ushawishi katika kuhamasisha umoja na ushirikiano baina ya wafanyakazi wa Chuo hicho.
Naye Kaimu Naibu Mkuu wa Ndaki hiyo Dkt. Coretha Komba, amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi kuendeleza umoja na ushirikiano kupitia matukio mbalimbali likiwemo Bonanza ili kuongeza ufanisi katika utendaji.
Dkt. Komba ameongeza kwa kusema kuwa Bonanza hilo limeamusha moyo wa kubuni mbinu za matukio endelevu ya kukutana wafanyakazi pamoja, huku akipendekeza Kamati iliyoandaa Bonanza hilo iwe ya kudumu ili kuendeleza majumuisho mengine ambayo watajipangia na kupendekeza.
Mshauri wa Wanafunzi na Mratibu wa Shughuli za Michezo Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bi Zitta Victoria Mnyanyi, amesema kuwa kupitia Bonanza hilo wamejifunza vitu mbalimbali pamoja na kufurahishwa na Mazingira ya Msitu wa Asilia Pugu Kazimzumbwi, huku akieleza kuwa wataendelea kuratibu matukio ya aina hiyo ambayo yataongeza umoja, upendo na utendaji kazi wa pamoja.
Kwa upande wa Wafanyakazi wa Ndaki hiyo, ambao waliungana na wachache kutoka Makao Makuu ya Mzumbe Morogoro, wameonyesha kufurahishwa sana na Bonanza hilo na kupongeza waandaaji kwa kuwajengea uwezo.
“Kwa kweli tumefurahishwa sana na mazingia ya huku Pugu, Kazimzumbwi pamoja yale tuliyoyafanya leo, Tunaipongeza Serikali kwa ubunifu mzuri na uamuzi wa kulinda hifadhi ya Msitu huu.”
Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa vyuo vikuu Bora nchini ambapo wanaongozwa na kauli mbiu inayosema: “TUJIFUNZE KWA MAENDELEO YA WATU”