Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika Hafla ya Kuwaaga Watumishi wa Wizara hiyo waliostaafu Utumishi wa Umma, iliyofanyika jijini Dodoma, Februari 2, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya, akizungumza katika Hafla ya Kuwaaga Watumishi wa Wizara hiyo waliostaafu Utumishi wa Umma, iliyofanyika jijini Dodoma, Februari 2, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Huduma za Uangalizi Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Aloyce Musika, akizungumza kwa niaba ya Watumishi wote waliostaafu Utumishi wa Umma katika Wizara hiyo, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa hao waliostaafu kazi hivi karibuni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimkabidhi zawadi ya pongezi kwa Mkurugenzi wa Huduma za Uangalizi Mstaafu wa Wizara hiyo, Aloyce Musika (kulia), kwa kustaafu kazi hivi karibuni, katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika, jijini Dodoma, Februari 2, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camilius Wambura akimpongeza Kamishna wa Polisi, Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Kambi na Makazi, Nsato Marijani kwa kustaafu kazi hivi karibuni, katika hafla ya kuwaaga watumishi waliostaafu Utumishi wa Umma wa Wizara hiyo, katika hafla iliyofanyika, jijini Dodoma, Februari 2, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikata keki iliyoandaliwa kwa ajili ya Watumishi wa Wizara waliostaafu utumishi wa umma, katika hafla ya kuwaaga watumishi waliostaafu Utumishi wa Umma wa Wizara hiyo, katika hafla iliyofanyika, jijini Dodoma, Februari 2, 2024. Wapili Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), akiwaongoza viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi, kucheza wimbo unaoimbwa na Katibu Muhtasi, Rebecca Mnahela (kushoto), wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi waliostaafu Utumishi wa Umma wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, Februari 2, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………………
Na Mwandishi Wetu, MoHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewapongeza watumishi wastaafu wa Wizara yake kwa mchango mkubwa walioutoa katika kuutumikia umma na kutoa rai kwa watumishi wanaobakia kukumbuka mazuri hayo na kuyaenzi.
Masauni ametoa kauli hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu kumi wa Wizara yake iliyofanyika Februari 2, 2024 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Kaspar Mmuya, Wakuu wa Vyombo vya Usalama pamoja na Watumishi wa Wizara hiyo.
‘Njia nzuri ya kuwaaga wenzetu ni kufurahi pamoja ili tubaki na kumbukumbu nzuri na wao waondoke wakiwa na kumbukumbu nzuri,’ alisema Masauni.
Alisema wastaafu wanatakiwa kujua kwamba kustaafu utumishi wa umma sio kutelekezwa na Serikali bali ni kuingia katika mfumo wa kujipatia kipato mwenyewe na kuondoka katika mfumo wa kuajiriwa.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya, amesema dhumuni la sherehe hiyo ni kuwapongeza wastaafu hao na kutambua mchango mkubwa waliufanya katika kipindi chote walichokua wanatumikia umma na kuwatakia heri katika maisha mapya wanayokwenda kuyaanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi Mstaafu, Aloyce Musika, kwa niaba ya wastaafu wenzake, amesema wanaishukuru Serikali kwa bahati waliyoipata ya kulitumikia Taifa.
‘Watanzania tupo zaidi ya milioni sitini, tunashukuru kuwa miongoni mwa wachache waliochaguliwa kulitumikia taifa hili na tumetimiza majukumu yetu kikamilifu,’ alisema Musika.
Pia, alimpongeza Waziri Masauni, kwa kuiongoza Wizara hiyo kwa weledi mkubwa ikiwamo kutatua changamoto mbalimbali zilizokua zikiikabili wizara hiyo hususani upungufu wa Bajeti ya Wizara hiyo.