Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mratibu Mwandamizi wa Utafiti Neema Tindamanyire wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 31, 2024, Jijini Dar es Salaam kuhusu ufadhili wa miradi ya utafiti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 31, 2024, Jijini Dar es Salaam kuhusu ufadhili wa miradi ya utafiti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Afisa Mratibu Mwandamizi wa Utafiti COSTECH, Neema Tindamanyire, akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 31, 2024, Jijini Dar es Salaam kuhusu ufadhili wa miradi ya utafiti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mratibu Mwandamizi wa Utafiti Neema Tindamanyire wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 31, 2024, Jijini Dar es Salaam kuhusu ufadhili wa miradi ya utafiti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imewataka watafiti nchini kuandaa andiko la utafiti Jumuishi (Inter – disciplinary / multidisciplinary research proposal) ili kufanya tafiti zenye kuleta tija na kuweza kuchangia kuleta suluhu na uelewa wa changamoto zitakanazo na mabadiliko ya Tabia ya nchi.
Miradi hiyo ya utafiti imefadhiliwa na COSTECH kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Nchini Norway, Norad iitwayo ‘COSTECH Climate Change Research Program’ kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya utafiti wa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa miaka mitano ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 31, 2024, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu, amesema kuwa miradi itakayofadhiliwa ni miradi mkubwa ambapo kila mradi unategemewa kugharamiwa kuanzia shilingi milioni mia mbili na ishirini hadi milioni mia sita kwa muda wa miaka minne.
Dkt. Nungu amesema kuwa miradi inayofadhiliwa ni mikubwa hivyo watafiti watahitajika kushirikiana na watafiti kutoka pande zote za Tanzania (Bara na Visiwani).
“Ili kuhakikisha watafiti wanakuwa na uelewa mzuri COSTECH tumeandaa warsha itakayofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 1/2/2024, lengo ni kujenga ufahamu na uelewa kwa watafiti wetu ili waweze kuandaa maandiko mazuri na shindani” amesema Dkt. Nungu.
Dkt. Nungu amesema kuwa ni fursa kwa watafiti wote nchini kujisajili kwa njia ya mtandao ili waweze kuhudhuriwa warsha na kupata fursa ya kuuliza maswali na kueleza changamoto walizonazo katika kuandaa maandiko yao.
Ameeleza kuwa warsha hiyo itarekodiwa ili kuwawezesha ambao hawataweza kuhudhuriwa waweze kupata taarifa ambayo itawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Dkt. Nungu amesema kuwa pia wanatarajia kuingia makubaliano mengine na Serikali ya Sweden (Sida) February 2024 kwa ajili ya kufadhili shughuli za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) kwa miaka mitano ijayo.
Afisa Mratibu Mwandamizi wa Utafiti
COSTECH, Neema Tindamanyire, amesisitiza umuhimu watafiti kutuma maandiko yao pamoja na kushiriki katika warsha ya mtandao.