Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akisalimia Viongozi na Wanachama alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE Mkoa wa Dar Es Salaam.
Wanachama na Viongozi Mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE Mkoa wa Dar Es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akizungumza na Viongozi na Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi za CCM kwa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE patika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
Wanachama Wapya wakila Kiapo Cha Chama.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndg. Abasi Mtemvu, akizungumza na Viongozi na Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akizungumza na Viongozi na Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.(Picha na Fahadi Siraji wa CCM)
………
Na Sophia Kingimali.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa rai kwa vijana kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo ili kuongeza vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo januari 20,2024 jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Kanali Abdulrahman Kinana katika mkutano Mkuu maalumu wa ukaribisho wa Wananchama wapya 1,167 seneti ya vyuo vikuu tawi la DIT, CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila kata ya Upanga Mashariki.
Amesema Chama kitajitahidi kuwapitisha vijana kwa wingi kwenye kugombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya mtaa.
“Chama kinawategemea sana vijana kwani ndio chachu ya mawazo ya Chama hivyo wasifikiri kuwa kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka hivyo watambue kuwa wao ni taifa la leo.Amesema Kinana.
Amesema Chama kinawategemea vijana kwa ushauri, kujenga hoja na kukosoa hivyo watambue wao ni watu wa kisasa wasomi kwa sababu wanapata rasmi na inayotokana na mitandao ya kijamii .
” Kutokana na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri , kitujenga na kutukosoa tunawategemea sana, toeni mawazo, mwaka huu tuna Uchaguzi wa serikali za Mitaa, nawasihi vijana wa vyuoni jitokezeni na gombeeni kwa nafasi zote mwaka huu,” amesema
Kinana amesema Chama hicho ni kikibwa hivyo wanapaswa kukilinda, kujipanga,kuweka mikakati na kugawa majukumu.
Amesema yapo mambo yanayochangia kukipa ushindi Chama hicho kuwa ni utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM, hivyo amewataka vijana hao kuchagua viongozi wenye uwezo sio wa kubebwa wala kutumia fedha kupata nafasi kwani Hata Rais Dk.Samia ameahidi hakuna mtu atakayebebwa bali atachaguliwa kutokana na sifa zake.
Sambamba na hayo Kinana ameahidi kutoa kompyuta,machine ya kuchapishia na printa kwa seneti ya vyuo vikuu mkoa wa Dar es salaam.
NAYE,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu amesema katika kuhakikisha seneti imaweza kusimama yenyewe na kujitegemea Ofisi ya mkoa watachangia sh.milioni 2 kwenye mfuko wa vijana zitakazochangia kununua vitu vitakavyowawezesha kujitegemea.
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema wanatarajia wanachama hao wapya ambao ni wasomi wataenda kuyasemea mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk.Samia.
“Hatua hii inaonyesha jinsi Rais Dk.Samia anavyofanya vizuri na kugusa nyoyo za Watanzania hivyo sasa Ilala tunaanza rasmi ajenga ya Samia ya mwaka 2025 kuleta ushindi na ushindi ni lazima”Amesema Zungu.
Ameongeza kuwa katika chaguzi zinazotarajiwa 2024/2025 watambeba na kumtetea kiongozi anayesimamia umoja wa Watanzania na kubeba kero zao.
“Msibabaishwe wala msidanganywe na wasiokitakia mema Chama chetu na nchi yetu, hivyo Jimbo la Ilala tutachangia sh.milioni tano ili muweza kujisimamia na pia mikopo inayotewa na serikali msizubae mjiimarishe kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wasiostahili kuchukua mikopo,” amesema.
Aidha Zungu amewataka vijana hao kuachana na vitu vya anasa, vitakavyowapoteza muda bali watumie mitandao kufanyabiashara zao ili kujiongezea kipato.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amempongeza Kinana Kwa kuwa mlezi mzuri wa vijana na jinsi anavyofanya kazi anawapa nguvu ya kuendelea kuchapaka kazi.
“Hali ya siasa kwa wilaya ya Ilala na mkoa wa Dar es Salaam ni mzuri hivyo tunashukuru Kwa kuwa na viongozi wa Chama Wazuri na wachapakazi na juhudi zako kama mlezi wa vijana zinazidi kutuongezea hamasa ya kuchapa kazi,” Amesema Mpogolo.
Kwa upande wake, Katibu wa Seneti vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam, Mabula Mabula amemuomba mwenyekiti wa chama hiko Rais Dkt Samia Suluhu kuangalia namna ya kuwaongeza mikopo wanafunzi wa vyuo vya kati lakini pia kupata vitendea kazi ili waweze kujitegemea ambapo amevitaja vifaa hivyo ni compyuta,printer na mashine ya fotokopi.