MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameipongeza mahakama ya wilaya hiyo kwa kutenda haki kwenye kesi mbalimbali ambazo zinapelekwa kusikilizwa na kutolea hukumu.
Akizungumza katika wiki hii ya sheria, Moyo alisema kuwa tangu ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Nachingwea ameona mabadiriko makubwa ya kiutendaji katika mahakama ya wilaya ya Nachingwea.
Moyo alisema kuwa awali alipata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa hawatendewi haki na Mahakama hiyo lakini alipofaatilia aligundua kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea bado hawana uelewa wa sheria jambo linalowafanya wapoteze haki zao.
Alisema kuwa ameshuhudia kwa kipindi ambacho yupo Nachingwea mahakama hiyo imetenda haki na kutoa huku nyingi za haki huku kesi zikiendeshwa kwa kipindi kifupi.
Hata hivyo Moyo aliumba uongozi wa Mahakama ya wilaya ya Nachingwea kuendelea kutoa elimu ya sheria kwa wananchi hasa vijijini.