Na. Omar Hassan, Said Bakari – ZANZIBAR Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amesema upatikanaji wa vifaa vya kisasa katika Jeshi la Polisi kunachangia mageuzi makubwa ya matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi na kudumisha ustawi na usalama wa raia na mali zao.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Kumpyuta kumi na tatu (13) kutoka katika kampuni ya ASAS GROUP alisema vifaa hivyo vitaliwezesha Jeshi la Polisi kutoa huduma bora na kwa wakati kwa kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu na wahalifu.
Nae Mwakilishi kutoka ASAS GROUP Fahad Masoud Ali alisema Kampuni hiyo imetoa vifaa hivyo kwa Jeshi la Polisi ili Jeshi hilo liendelee kusimamia Amani na usalama uliopo na pia wanaunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussen Ali Mwinyi, za kuleta Maendeleo.