Akizungumza katika hafla hiyo Mhe Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga Maarufu Jah. People Amesema upo Umuhimu wa Polisi kuendelea kushirikiana na jamii kupitia Shughuli mbali mbali ili kuwezesha mahusiano mazuri baina yao na wananchi ili kupata taarifa sahihi hasa za kihalifu.
Jah People Amesema hayo wakati akiwapongeza Askari Polisi wastaafu wanne na kukaribisha maafisa 4 wapya katika Wilaya ya kipolisi ya Makambako ambao Walianza Kutoa Msaada kituo cha Kulelea Watoto Yatima Kilichopo Ilunda Kata ya Mtwango Wilayani Makambako na kutoa Mahitaji Muhimu vikiwemo vyakula.
Aidha Jah people Amewataka Wananchi kuwapa Ushirikano Wastaafu wanaporejea sehemu zao za Kuishi na kuomba Waendelee kutoa Ushirikiano kwa Maafisa wapya ambao wameingia kazini Makambako.
Akizungumza Mbele ya Mgen Rasmi Mkuu wa Polisi Wilaya Makambako SSP Omar M. Diwani amesema Wamejipanga vyema kuhudumia wananchi na Wataendeleza Mahusiano Mazuri kwa Wananchi ambapo tukio hilo Liliambatana na Bonanza la Michezo baina ya Police na Wananchi.
Aidha SSP Diwani Amesema Michezo ni Muhimu ili kuendelea kuimarisha afya na wananchi waipe kipaumbele ili kuimarisha afya zao na kujenga mahusiano mazuri na jeshi la Polisi kupitia michezo.
Diwani Amesema Wanatambua Hitaji la Wananchi wa Makambako na wameamua kwanza Ujenzi wa Jengo la Dawati la jinsia na watoto ili kutatua Migogoro ya Ndoa ambayo inaweza kuibua changamoto kubwa ya Watoto kushindwa kupata Haki zao za Msingi baada ya Wazazi kushindwa kuishi pamoja.
Amesema Jengo hilo litasaidia kupunguza makali ya Migogoro katika Wilaya hyo.
Jengo hilo halijakamilika bado linahitaji fedha Hivyo Mgen Rasmi ameongoza Harambee ya kuchangia Ujenzi wake ambapo zaidi ya shilingi Million 9 Zimekusanywa katika Hafla hiyo huku Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi ya Makambako akiwataka aadau wengine kujitokeza kuchangia kwa kuwa jumla ya fedha Inayohitajika ni Million 23 ili Kukamilisha Jengo hlo.