SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson,akizungumza wakati 
  akihitimisha mashindano ya Azania Bunge Bonanza yaliyoandaliwa na Benki ya Azania yaliyofanyika leo Januari 27,2024 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema katika jitihada za kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini watatumia mashindano yajayo ya  Bunge  Marathon kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya  wavulana.
Dkt.Tulia ametoa kauli hiyo leo Januari 27,2024 jijini Dodoma wakati  akihitimisha mashindano ya Azania Bunge Bonanza yaliyoandaliwa na Benki ya Azania.
Mhe.Tulia amesema kuwa tayari bunge limeshajenga shule maalum ya wasichana iliyopo eneo la Kikombo jijini Dodoma na walijenga kwa kutumia pesa za mashindano ya riadha.
“Mashindano ya riadha yajayo yatatumika kukusanya  fedha kwa ajili ya kujenga shule  maalum ya  wavulana hivyo tutangaza wapi shule hiyo itajengwa,hii ni kutokana na kuwa bunge letu lina wanaume hivyo tutajenga pia shule ili tuwe na shule mbili ya wasichana na wavulana.
Pia ameipongeza Benki ya Azania kwa kuandaa bonanza hilo kwa wabunge na pia amewashukuru washindi waliopatikana kama mashindano hayo.
“Napongeza tamasha la michezo kwa Wabunge,Watumishi pamoja na hamasa kubwa iliyofanywa na Yanga SC chini ya Afisa habari wetu Ali Kamwe”amepongeza Dkt.Tulia
Mashindano ya Azania Bunge Bonanza  yamedhaminiwa na Azania Bank ambapo yamewakutanisha mashabiki wa timu ya Simba na Yanga ikiwa ni Wabunge na wafanyakazi wa bunge.
Katika Mpira wa Miguu timu ya wabunge wa Yanga SC  wameibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya wabunge wa Simba SC kwa Mikwaju ya Penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa kufungana bao 1-1.
Wabunge wanawake wapenzi wa Yanga na Simba na baadhi ya watumishi wa Bunge wakishindana kula ubwabwa maharage katika wakati wa Azania Bunge Bonanza kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Januari 27, 2024.Bonanza hilo lililofana limedhaniwa na Benki ya Azania.
Wabunge wanawake wapenzi wa Yanga na Simba na baadhi ya watumishi wa Bunge wakishindana kula ubwabwa maharage katika wakati wa Azania Bunge Bonanza kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Januari 27, 2024. Bonanza hilo lililofana limedhaniwa na Benki ya Azania.